Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst)
Mhe. George Mkuchika (Mb), akifungua mjadala kuhusu Kuelekea Msimamo wa Pamoja wa Afrika kuhusu
Urejeshwaji Mali wakati wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya
Rushwa Barani Afrika iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la
Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb), alipokuwa
akifungua mjadala kuhusu Kuelekea Msimamo wa Pamoja wa Afrika kuhusu
Urejeshwaji Mali wakati wa kongamano hilo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani akitoa maelezo ya awali kuhusu Siku Maalumu ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika wakati wa Kongamano la siku hiyo iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akimkabidhi mwongozo wa utendaji kazi mmoja wa wajumbe wa kamati ya uadilifu ya Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akipokea hati ya utambuzi wa mchango wake katika mapambano dhidi ya rushwa toka kwa viongozi wa Klabu ya Wapinga Rushwa ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu
Serikali haitosita
kumchulia hatua za kisheria mtu yeyote bila kujali wadhifa alionao pindi
atakapobainika kujihusisha na masuala ya rushwa ambayo ni kikwazo kwa maendeleo
ya taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) alipokuwa
akifungua mjadala kuhusu “Kuelekea Msimamo wa Pamoja wa Afrika kuhusu
Urejeshwaji Mali” wakati wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya
Rushwa Barani Afrika iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.
Mhe. Mkuchika amesema,
baadhi ya watu wanadhani kuwa, Serikali inashughulika na wala rushwa wadogo
wadogo tu, ukweli ni kwamba, wapo baadhi ya walioshika nyadhifa za uwaziri
wamelazimika kuwajibika na kutumikia kifungo kutokana na suala la rushwa na
ubadhirifu wa mali za umma.
Mhe. Mkuchika ameongeza
kuwa, hatua dhidi ya waliobainika na masuala ya rushwa ni matokeo ya
uanzishwaji wa Mahakama ya wala rushwa na wahujumu uchumi iliyoanzishwa, ikiwa
ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Tumeanza kupiga hatua
katika mapambano dhidi ya rushwa na matokeo yameonekana, hivyo tusibweteke kwasababu
bado tuhahitaji kuendeleza mapambano hayo,” Mhe. Mkuchika amesisitiza.
Mhe. Mkuchika
ameipongeza Klabu ya Wapinga Rushwa ya Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuwa hai na
yenye nguvu katika mapambano dhidi ya rushwa, na kutoa wito kwa klabu nyingine katika
taasisi za elimu ya juu kuiga mfano huo.
Aidha, Mhe. Mkuchika
amewahimiza wanataaluma nchini, klabu za wapinga rushwa katika vyuo vya elimu
ya juu, TAKUKURU pamoja na wadau wengine kuendelea kufanya tafiti kuhusu rushwa
na masuala ya utawala bora ili kutoa mapendekezo ya namna Serikali na wananchi
watakavyoshiriki katika mapambano dhidi ya rushwa.
Mada kuhusu historia
ya vita dhidi ya rushwa Tanzania na urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia
ya rushwa barani Afrika ziliwasilishwa katika kongamano hilo.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 19 JUNI, 2019
No comments:
Post a Comment