NA
TIGANYA VINCENT
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa
wito kwa wafanyabiashara kujenga tabia ya kutoa risti na kuweka kumbukumbu za
mauzo wanayofanya kwa ajili ya kuwa na taarifa sahihi zitakazokazosaidia kuwa na
makadirio yatakayo toa picha halisi ya kodi wanazotakiwa kulipa kwa mwaka.
Hatua itasaidia kuondoa mvutano kati ya
wafanyabiashara na Maofisa wa TRA wakati wa ukadiriaji wa Kodi ambazo
watakiwa kulipa na kuiwezesha Serikali kupata Kodi inayotakiwa.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa
TRA Mkoa wa Tabora Thomas Masese wakati wa semina ya uelimishaji
wafanyabiashara wa Wilaya mbalimbali za Mkoa huo.
Alisema baadhi ya wafanyabiashara wanapouza
bidhaa kwa wateja hawatoi stakabadhi na wengine hawaweki kumbukumbu za mauzo ya
kila siku jambo linalosababisha ugumu kwa Maofisa wa TRA kujua mauzo halisi.
Masese alisema wafanyabiashara wa aina
hiyo wanapokadiriwa Kodi wanalalamika kuwa wanaonewa ,wakati wangekuwa wanatoa stakabadhi
wasikuwa na mvutano na Maofisa wa TRA.
“ Ndugu ili kuondoa mvutano wakati wa
ukadiriaji wa kodi ni vema mkatoa risti na kuweka kumbukumbu za mauzo yenu ya
kila siku…yatatusaidia kujua mauzo yako kwa mwaka na kodi ambayo mnapaswa
kulipa” alisema.
Naye Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipa
Kodi wa TRA Mkoa wa Tabora Geofrey Comoro aliwataka wafanyabaishara ambao wamesajiliwa
na kupewa Namba ya Mlipa Kodi (TIN namba) ambao biashara zao zimeyumba kuandika
barua ili Maofisa wa TRA wafike kwao kuona hali halisi.
Alisema
kitendo cha kutoa taarifa , TRA itaendelea kumuhesabu kama
mfanyabiashara anayepaswa kulipa kodi kama ilivyokuwa siku za awali.
No comments:
Post a Comment