NA
TIGANYA VINCENT
MENEJA Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
wa Tabora Thomas Masese amesema anatarajia kuweka kambi Wilayani Sikonge
kutatua kero mbalimbali zinawakabili wafanyabiashara wakati wa ulipaji kodi.
Hatua inalenga kuondoa mvutano kati ya
wafanyabiashara na watumishi wa TRA na kuongeza makusanyo ya Serikali.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa
TRA Mkoa wa Tabora Thomas Masese wakati wa semina ya uelimishaji
wafanyabiashara wa Wilayani Sikonge iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Alisema anataka atumie muda mwingi wa
kusikiliza kero na matatizo ya mfanyabiashara mmoja baada ya mwingine ili kujua
vikwazo mbalimbali vinavyowakabili kwa ajili kuleta mahuasiano mazuri yatakayosaidia ukusanyaji wa mapato.
Masese
alisema kutumia njia ya semina
pekee hakuwezi kumaliza matatizo ya wafanyabiashara wote kwa sababu muda
ni mfupi na wafanyabiashara wengi bado walitaka kueleza shida
zinawakwaza wakati wa ulipaji kodi.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akifungua semina ya siku mmoja ya wafanyabiashara wa Sikonge aliwaonya
Maofisa wa TRA ambao wanatumia lugha zisizofaa wakati wa utoaji wa huduma kwa
wateja.
Alisema ni muhimu kujenga mahusiano
mazuri ambayo yatasaidia ukusanyaji wa Kodi za Serikali kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za maendeleo ikiwemo uboreshaji wa huduma za afya , maji na
barabara.
No comments:
Post a Comment