June 17, 2019

VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA TISHIO KWA WATOTO WILAYANI PANGANI


KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange akizungumza wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya Kata ya Pangani Mashariki iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa) wilayani Pangani ambapo Halmashauri wa wilaya hiyo ilishirikiana na Shirika la Uzikwasa.

MKURUGENZI wa Shirika la UZIKWASA Novatus Urrasa akizungumza wakati wa wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya Kata ya Pangani Mashariki iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa) wilayani Pangani ambapo Halmashauri wa wilaya hiyo ilishirikiana na Shirika la Uzikwasa.

AFISA Maendeleo ya Jamii wilaya ya Pangani Elias Msuya akizungumza wakati wa siku ya Mtoto wa Afrika.

Mwanafunzi wa shule ya Msingi Funguni Aisha Ally akisoma risala.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD), Georgina Matagi akizungumza na vikundi mbalimbali.

KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange katika akizindua Mpango wa Taifa kazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) wakati wa Tamasha la Ugawaji tuzo kwa vijiji bora katika mapambano dhidi ya Ukatili wa wanawake na watoto wilayani humo kushoto ni Mkurugenzi wa UZIKWASA Novatus Urassa.
Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia matukio.
 
Pangani, Tanga

VITENDO vya ubakaji na Ulawiti ikiwemo wanafunzi kupewa ujauzito ni moja ya vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa tishio kwa watoto wilayani Pangani huku ikielezwa kwamba wanaofanyiwa vitendo hivyo wanaanzia darasa la pili na kuendelea jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa maendeleo yao

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya Kata ya Pangani Mashariki iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa) wilayani Pangani ambapo Halmashauri wa wilaya hiyo ilishirikiana na Shirika la Uzikwasa.

Alisema hilo limekuwa ni tatizo kubwa sana wilayani humo huku akiitaka jamii kubadilika na kuachana na vitendo vya namna hiyo kwani vimekuwa vikikwamisha watoto kushindwa kufikia ndoto zao.

“Hili ni tatizo kubwa sana OCD hapa wilayani Pangani lakini pia inaumiza sana hivyo jamii lazima ibadilike na kuhakikisha wanawafuchua watu wanaohusika na vitendo hivyo kwenye jamii lakini pia toeni ushirikiano tuweze kumaliza matukio ya ukatili wa kijinsia kiu yangu ni kuona matokeo kesi zinaendelea mahakamani yanakwisha na wahusika kuchukuliwa hatua “Alisema

Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano wa kwenda kutoa ushahidi pindi yanapotokea matukio hayo msikubali kurubuniwa kwani kufanya hivyo tunapelekea haki kushindwa kutendeka na wahusika kuchukuliwa hatua.

“Lakini kama mashauri mengi yatakuwa yanalalamikiwa na mashauri kushindwa kupata muafaka hiii pia sio taswira nzuri kwetu hivyo watu kwenye vyombo husika wananchi watajenga mashaka nao nao wabadilike “Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi aliwataka wanaume kuwaacha watoto wa kike wasome na kupata elimu ambayo itakuwa ndio silaha kubwa kwenye maisha yao ya sasa na baadae.

Hata hivyo aliwataka watendaji wa Kata na Vijiji kuacha kumaliza kesi zinazohusiana na masuala hayo kwenye maeneo yao badala yake wahakikishe zinafikishwa mahakamani.

Naye kwa upande wake Mwanafunzi wa shule ya Msingi Funguni Aisha Ally aliziomba mamlaka husika za kisheria kuhakikisha zinawachukulia hatua kali za kisheria watu wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji, ulawiti na wanaowapa mimba wanafunzi kwani wanakatisa ndoto zao.

Huku wakieleza kwamba watafurahi siku moja itatokea wabakaji au wanaowalawiti wakifungwa vifungo mbalimbali kwani hivi sasa kesi ni nyingi lakini matokeo ya kesi ni madogo sana.

Siku hiyo ilikwenda sambamba na sambamba na kauli mbiu isemayo mtoto ni msingi wa Taifa endelevu tutumze, tumlinde na tumuendeleze ambapo alisema siku hizi kumekuwa na tabia ya watoto katika jamii kubakwa na kulawitiwa na watu wazima ikiwemo wengine kuwaozesha tabia ni kiyume cha sheria ya nchi.

Alisema tabia hizo zimekuwa kikwazo kikubwa cha watoto hao na wengi kushindwa kuhitimu masomo yao na kupata mimba za utotoni na kupelekea wimbi la utegemezi kwenye familia na Taifa kwa ujumla ikiwemo kuongezeka magonjwa ya zinaa na kusababnisha kupungua nguvu kubwa ya Taifa.

“Sisi kama watoto tuna ndoto nyingi na serikali ndio kimbilio letu baada ya wazazi na walezi na jamii kukatisha ndoto zetu ,jamii itambue kumekuwa na wimbi kubwa la kubakwa na kulawitiwa watoto wa kiume wao na watu wazima hivyo tunaimba jamii ikishiriki kikamilifu kutulinda kututunza na kutuelendeleza kufikia malengo”Alisema

No comments:

Post a Comment

Pages