June 17, 2019

WAFANYABIASHARA WAHAKIKISHIWA USALAMA KATIKA BIASHARA ZAO

 Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB Makao Makuu, Donatus Richard, akizungumza na wajasiriamali na wafanyabiashara ambao ni wajumbe wa NMB Business Club ya mkoani Mwanza, wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo wajumbe hao. Kushoto ni Mwenyekiti wa Club hiyo anayemaliza muda wake, Mathiasi Rwechungura na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Godfrey Mzava.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, akizungumza na wajasiriamali na wafanyabiashara ambao ni wajumbe wa NMB Business Club ya mkoani Mwanza, jinsi walivyojipanga kuwalinda watu, mali na biashara zao wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo wajumbe hao,kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Godfrey Mzava na Mkuu wa kitengo cha Biashara wa NMB Makao Makuu Donatus Richard. (kulia).
 
 
Na Mwandishi Wetu
 
MKUU wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Jumanne Murilo amewahakikisha usalama wa pesa na mali zao.Akizungumza na  wafanyabiashara katika Jukwaa la business club,Jeshi lake limejipanga imara kuhakikisha wanafanyabiashara hawasumbuliwi na wahalifu.

 Aliwaomba wafanyabiashara mkoani hapa kuhakikisha wanatumia vyema jukwaa la Business Club katika kuhakikisha wanajenga uchumi imara wa nchi.
'"tumejipanga na tunapambana kuzuia uhalifu kabla haujatokea kuliko kukabiliana nao ukishatokea " Murilo alisema.

Alisema wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi bali wahakikishe wanafanya biashara zao kwa uhuru kwakuwa jeshi lake limejipanga vyema kuhakikisha hakuna masuala ya uhalifu.
Kwa upande wake,mkuu wa kitengo cha Biashara cha benki ya NMB makao makuu,Donatus Richard alisema benki yao itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kupitia ‘Business Club’

Alisema kupitia elimu watakazokuwa wanatoa kwa wafanyabiashara zitakuwa zikiwasaidia sana wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku.

Donatus alisema kwa sasa benki yao itaendelea kuwa karibu na wateja wao na alisema wataendelea kutoa mafunzo mbali mbali kwa wateja wao yakiwemo masuala ya masoko pamoja na kodi.

Alisema semina zao pia zimewasaidia wateja wao kuwa karibu na wateja wenzao ambapo jambo linalodumisha uhusiano mwema katika ufanyaji biashara zao.

Alisema kwa sasa benki yao ipo katika mikakati ya kuwapeleka wafanyabiashara 10 nchini China kwajili ya kuwenda kujifunza mambo ya kibiashara katika tamasha la biashara litakalo fanyika nchini humo katika mwezi wa 10, mwaka huu. Mmoja ya wafanyabiashara, Kejja Misungwi, alisema anaiomba benki ya NMB kuhakiksha wanaendelea kutoa semina za mara kwa mara kwa wateja wao jambo ambalo litawasaidia wateja kupata elimu za biashara zitakazowawesha upatakinaji wa faida katika biashara zao.

No comments:

Post a Comment

Pages