July 18, 2019

CMSA yazindua shindano kwa wanavyuo,Taasisi za elimu ya juu

Na Mwandishi Wetu
 
MAMLAKA ya Masoko mitaji na Dhamana (CMSA) imetangaza shindano la Masoko ya Mitaji kwa mwanafunzi wa vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya juu (CMUHLC) baada ya kuvunja rekodi kila mwaka.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama alisema, toka kuanzishwa kwa shindano hilo mwaka 2015/16 wamevuka lengo ambapo walipoanza lengo ilikuwa ni watu 2,000 lakini waliongezeka mpaka 7,500.

Mkama alisema mwaka 2016/17 lengo ilikuwa watu 7,000 ikawa 7,901, 2017/18 lengo watu 10,000 ikawa 15,000.

Alisema kutokana na malengo hayo kufanikiwa kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na watu 16,000 kwani wanaimani idadi hiyo inaweza kuzidi kutokana na takwimu kuwa juu kila mwaka, ambapo washindi watapewa zawadi ya pesa taslimu ikiwa na lengo la fedha hizo kuzitumia kuanzisha uwekezaji katoka masoko ya mitaji kwa kununua hisa, vipande vya uwekezaji wa pamoja au hati fungani.

Aidha Mkama aliwataka wanafunzi walioudhuria katika uzinduzi huo kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa shindano hilo kwa kutoa taarifa sahihi juu ya shindano hilo, linaliwapa fursa jinsi zote kushiriki.

CMSA  imezindua shindano hilo, ikiwa na kauli mbiu isemayo "Nafasi ya Masoko ya Mitaji na dhamana katika kupunguza umasikini na kuwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025," ikiwa na lengo la kutoa ajira kwa vijana.

"Imani yangu kubwa kwa nyie wanafunzi baadhi mlioudhuria hapa, mtafikisha vyema elimu hii ya shindano hilo ambalo litashindaniwa kwa njia ya kujibu maswali au kuandika insha na mshiriki anaruhusiwa kushiriki kwa njia hizo zote,"alisema.

Aidha Mkama aliwataka washiriki kuchangamkia fursa hiyo huku akiwapongeza washiriki wote walioshinda shindano hilo miaka iliyopita, kwani kupitia shindano hilo wameweza kusonga mbele na kujikwamua kimaisha.

Alisema shindano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mamlaka wa miaka mitano kuanzia 2018/19-2020/23 ambao pamoja na mambo mengine umetilia mkazo sekta ya Masoko ya Mitaji Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali.

"Pia mkakati huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa sekta ya Masoko ya Mitaji katika mpango wa Kitaifa wa huduma jumuishi za kifedha 2018-2022 unaolenga kuongeza ushiriki wa umma katika huduma za kifedha hususani kuweka katika masoko ya Mitaji,"alisema Mkama.

Alisema, wanavyuo ni kundi muhimu mamkubwa katika jamii ambalo ndiyo viongozi, wazazi na wawekezaji wa siku za usoni, na pia ni kundi muhimu katika familia, hivyo kwa kutambua umuhimu na thamani ya wanavyuo ndiyo sababu ya kuanzisha shindano hilo ili kutoa fulsa kwa wanavyuo kupata elimu ya Masoko ya mitaji na kuanza kujenga utamaduni wa kuweka akina kwa njia endelevu wakati wakiwa vyuoni.

Mkama alisema, elimu hiyo pia itasaidia kupunguza kushiriki katika fursa za uwekezaji za kitapeli na udanganyifu ambazo siku za usoni kumekua na wimbo kubwa kwa vijana kulagaiwa.
Aliongeza kuwa shindano hilo linashirikisha wanavyuo wote wa Tanzania Bara Visiwani kwa kuandika Insha na kujibu maswali yanayopita dhana ya Masoko ya mitaji na masoko ya bidhaa, kwani wanajivunia shindano hilo kutokana na kuwavutia washiriki wengi.
" Washindi wa shindano hilo wamepata fursa ya kujifunza kwa kitendo na kuongeza weledi katika masuala ya Masoko ya mitaji na imewezesha baadhi ya washiriki hao kupata nafasi za ajira katika kampuni za ushauri na ushiriki katika masoko ya Mitaji.mafunzo haya pia yamewezesha baadhi ya washiriki kutambua fursa na kuwawezesha kutengeneza nafasi za ajira na biashara katika sekta hii,"alisema na kuongeza kuwa lengo lao CMSA ni kuhakikisha mwaka 2022 wawe wametimiza lengo la kuwa fika Watanzania kwa asilimia 50 waweze kupata elimu juu ya Masoko ya mitaji.

No comments:

Post a Comment

Pages