Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Masoko mitaji na Dhamana (CMSA) imetangaza shindano la Masoko ya
Mitaji kwa mwanafunzi wa vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya juu (CMUHLC)
baada ya kuvunja rekodi kila mwaka.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama
alisema, toka kuanzishwa kwa shindano hilo mwaka 2015/16 wamevuka lengo
ambapo walipoanza lengo ilikuwa ni watu 2,000 lakini waliongezeka mpaka
7,500.
Mkama alisema mwaka 2016/17 lengo ilikuwa watu 7,000 ikawa 7,901, 2017/18 lengo watu 10,000 ikawa 15,000.
Alisema
kutokana na malengo hayo kufanikiwa kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na
watu 16,000 kwani wanaimani idadi hiyo inaweza kuzidi kutokana na
takwimu kuwa juu kila mwaka, ambapo washindi watapewa zawadi ya pesa
taslimu ikiwa na lengo la fedha hizo kuzitumia kuanzisha uwekezaji
katoka masoko ya mitaji kwa kununua hisa, vipande vya uwekezaji wa
pamoja au hati fungani.
Aidha
Mkama aliwataka wanafunzi walioudhuria katika uzinduzi huo kuhakikisha
wanakuwa mabalozi wazuri wa shindano hilo kwa kutoa taarifa sahihi juu
ya shindano hilo, linaliwapa fursa jinsi zote kushiriki.
CMSA
imezindua shindano hilo, ikiwa na kauli mbiu isemayo "Nafasi ya Masoko
ya Mitaji na dhamana katika kupunguza umasikini na kuwezesha Tanzania
kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025," ikiwa na lengo la kutoa
ajira kwa vijana.
"Imani
yangu kubwa kwa nyie wanafunzi baadhi mlioudhuria hapa, mtafikisha
vyema elimu hii ya shindano hilo ambalo litashindaniwa kwa njia ya
kujibu maswali au kuandika insha na mshiriki anaruhusiwa kushiriki kwa
njia hizo zote,"alisema.
Aidha
Mkama aliwataka washiriki kuchangamkia fursa hiyo huku akiwapongeza
washiriki wote walioshinda shindano hilo miaka iliyopita, kwani kupitia
shindano hilo wameweza kusonga mbele na kujikwamua kimaisha.
Alisema
shindano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mamlaka wa
miaka mitano kuanzia 2018/19-2020/23 ambao pamoja na mambo mengine
umetilia mkazo sekta ya Masoko ya Mitaji Tanzania ikiwa ni pamoja na
kutoa elimu kwa makundi mbalimbali.
"Pia
mkakati huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa sekta ya Masoko ya
Mitaji katika mpango wa Kitaifa wa huduma jumuishi za kifedha 2018-2022
unaolenga kuongeza ushiriki wa umma katika huduma za kifedha hususani
kuweka katika masoko ya Mitaji,"alisema Mkama.
Alisema,
wanavyuo ni kundi muhimu mamkubwa katika jamii ambalo ndiyo viongozi,
wazazi na wawekezaji wa siku za usoni, na pia ni kundi muhimu katika
familia, hivyo kwa kutambua umuhimu na thamani ya wanavyuo ndiyo sababu
ya kuanzisha shindano hilo ili kutoa fulsa kwa wanavyuo kupata elimu ya
Masoko ya mitaji na kuanza kujenga utamaduni wa kuweka akina kwa njia
endelevu wakati wakiwa vyuoni.
Mkama
alisema, elimu hiyo pia itasaidia kupunguza kushiriki katika fursa za
uwekezaji za kitapeli na udanganyifu ambazo siku za usoni kumekua na
wimbo kubwa kwa vijana kulagaiwa.
Aliongeza kuwa shindano hilo
linashirikisha wanavyuo wote wa Tanzania Bara Visiwani kwa kuandika
Insha na kujibu maswali yanayopita dhana ya Masoko ya mitaji na masoko
ya bidhaa, kwani wanajivunia shindano hilo kutokana na kuwavutia
washiriki wengi.
" Washindi wa shindano hilo wamepata fursa ya
kujifunza kwa kitendo na kuongeza weledi katika masuala ya Masoko ya
mitaji na imewezesha baadhi ya washiriki hao kupata nafasi za ajira
katika kampuni za ushauri na ushiriki katika masoko ya Mitaji.mafunzo
haya pia yamewezesha baadhi ya washiriki kutambua fursa na kuwawezesha
kutengeneza nafasi za ajira na biashara katika sekta hii,"alisema na
kuongeza kuwa lengo lao CMSA ni kuhakikisha mwaka 2022 wawe wametimiza
lengo la kuwa fika Watanzania kwa asilimia 50 waweze kupata elimu juu ya
Masoko ya mitaji.
No comments:
Post a Comment