Ndege
maalum ya Jeshi la Kenya iliyobeba Dhahabu ya Tanzania iliyokamatwa
Kenya ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
Jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli atashuhudia makabidhiano hayo Ikulu Dsm kutoka kwa Mjumbe
Malalum wa Rais Wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata. PICHA NA IKULU.
Dhahabu ya Tanzania iliyokamatwa
Kenya ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
Jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli atashuhudia makabidhiano hayo Ikulu Dar es Salaam kutoka kwa Mjumbe
Maalum wa Rais Wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata.
Na Waandishi Wetu, MAELEZO
RAIS Dkt. John Magufuli aipongeza Serikali ya Kenya kwa
maamuzi yake ya kuirejeshea dhahabu zenye uzito wa kilo 35.34 zilizotoroshwa nchini
Tanzania na Wafanyabiashara wasio waamini kwa njia ya magendo mwaka 2018.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi dhahabu pamoja
na fedha taslimu akiwa pamoja na ujumbe wa Mawaziri na Watendaji wa Serikali ya
Kenya leo Jumatano (Julai 24, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema
kitendo kilichofanywa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni cha kizalendo na
kimedhirisha urafiki na undugu wa kweli baina yake na Tanzania.
Amesema kuwa Serikali ya Kenya kupita vya vyombo ulinzi na usalama
vimefanya kazi nzuri inayodhirisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya, na ameeleza kuwa kama kusingekuwepo na ushirikiano huo dhahabu
na pesa hizo zilizokamatwa kwenye uwanja
wa Jommo Kenyatta nchini humo visingelejeshwa Tanzania.
“Tunaipongeza Serikali
ya Kenya kupitia vyombo vya vyake vya ulinzi vilivyofanya kazi nzuri ya
kukamata dhahabu kilo 35.34 iliyokuwa imeshavuka kwenye mipaka yetu, na tuwapongeze pia kwa kutunza pesa yetu ambayo
ilibiwa Tanzania kwenye Benki ya NMB mwaka 2004, kwa kweli huu ni uaminifu
mkubwa” amesema Rais Magufuli.
Licha ya kuipongeza vyombo vya ulinzi vya Kenya Rais
Magufuli ameshangazwa na ukimya kutaka
vyombo vya ulinzi vya Tanzania na hivyo kuvitaka kujitafakari kwa namna dhahabu
hiyo ilivyoweza kukamatiwa Kenya na Sio
Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo
watuhumiwa walitumia ndege ya ‘Precision Air’ kusafirisha mzigo huo.
“Vyombo vyetu
vya ulinzi vipo hapa lazima niviseme, dhahabu iliwezaje kufika Kenya tukashindwa
kuwakamata watumiwa wakiwa bado kwenye uwanja wa Mwanza?, hapa lazima vyombo
vyetu mjitafakari japo mnafanya kazi kubwa lakini ikiwezekana mkajifunze kwa
wenzenu wawape mbinu walizozitumia katika hili” amesema Rais Magufuli.
Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia alimpigia simu ya moja kwa moja Rais Uhuru Kenyatta
na kutoa shukrani zake na kumdhibitishia kuwa amepokea mzigo huo na kumpongeza
kwa ushirikiano wa Serikali yake kwa Watanzania, ambapo Rais Kenyatta akimuhakikishia
Rais Magufuli ushirikiano wa kudumu ambao utachochea zaidi maendeleo kama
walivyohaidi na kupewa mamlaka na wananchi.
Naye mjumbe maalumu aliyemwakilisha Rais Kenyatta,
Monica Juma ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kenya amesema Serikali
ya Kenya itaendeleza ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya ulinzi na usalama
kwa kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza uchumi wa pande zote mbili.
Na kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi amesema Kenya na Tanzania
ni ndugu tokea ezi na enzi, hivyo Serikali Tanzania itahakikisha kuwa inaendelea
kushirikiana na Kenya ili kufanya ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi wa
nchi hizo.
No comments:
Post a Comment