HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 24, 2019

USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KENYA WAZIDI KUSHAMILI, MAMILIONI NA DHAHABU YAREJESHWA

 Ndege maalum ya Jeshi la Kenya iliyobeba Dhahabu ya Tanzania iliyokamatwa Kenya ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli atashuhudia makabidhiano hayo Ikulu Dsm kutoka kwa Mjumbe Malalum wa Rais Wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata. PICHA NA IKULU.
Dhahabu ya Tanzania iliyokamatwa Kenya ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atashuhudia makabidhiano hayo Ikulu Dar es Salaam kutoka kwa Mjumbe Maalum wa Rais Wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata. 



Na Waandishi Wetu, MAELEZO

RAIS Dkt. John Magufuli aipongeza Serikali ya Kenya kwa maamuzi yake ya kuirejeshea dhahabu zenye uzito wa kilo 35.34 zilizotoroshwa nchini Tanzania na Wafanyabiashara wasio waamini kwa njia ya magendo mwaka 2018.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi dhahabu pamoja na fedha taslimu akiwa pamoja na ujumbe wa Mawaziri na Watendaji wa Serikali ya Kenya leo Jumatano (Julai 24, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kitendo kilichofanywa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni cha kizalendo na kimedhirisha urafiki na undugu wa kweli baina yake na Tanzania.

Amesema kuwa  Serikali ya Kenya kupita vya vyombo ulinzi na usalama vimefanya kazi nzuri inayodhirisha ushirikiano uliopo  kati ya Tanzania na Kenya,  na ameeleza kuwa  kama kusingekuwepo na ushirikiano huo dhahabu na pesa  hizo zilizokamatwa kwenye uwanja wa Jommo Kenyatta nchini humo visingelejeshwa Tanzania.

“Tunaipongeza  Serikali ya Kenya kupitia vyombo vya vyake vya ulinzi vilivyofanya kazi nzuri ya kukamata dhahabu kilo 35.34 iliyokuwa imeshavuka kwenye mipaka yetu, na  tuwapongeze pia kwa kutunza pesa yetu ambayo ilibiwa Tanzania kwenye Benki ya NMB mwaka 2004, kwa kweli huu ni uaminifu mkubwa” amesema Rais Magufuli.

Licha ya kuipongeza vyombo vya ulinzi vya Kenya Rais Magufuli ameshangazwa na ukimya  kutaka vyombo vya ulinzi vya Tanzania na hivyo kuvitaka kujitafakari kwa namna dhahabu hiyo ilivyoweza kukamatiwa  Kenya na Sio Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  ambapo watuhumiwa walitumia ndege ya ‘Precision Air’ kusafirisha mzigo huo.

 “Vyombo vyetu vya ulinzi vipo hapa lazima niviseme, dhahabu iliwezaje kufika Kenya tukashindwa kuwakamata watumiwa wakiwa bado kwenye uwanja wa Mwanza?, hapa lazima vyombo vyetu mjitafakari japo mnafanya kazi kubwa lakini ikiwezekana mkajifunze kwa wenzenu wawape mbinu walizozitumia katika hili” amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia  alimpigia simu ya moja kwa moja Rais Uhuru Kenyatta na kutoa shukrani zake na kumdhibitishia kuwa amepokea mzigo huo na kumpongeza kwa ushirikiano wa Serikali yake kwa Watanzania, ambapo Rais Kenyatta akimuhakikishia Rais Magufuli ushirikiano wa kudumu ambao utachochea zaidi maendeleo kama walivyohaidi na kupewa mamlaka na wananchi.

Naye mjumbe maalumu aliyemwakilisha Rais Kenyatta, Monica Juma ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kenya amesema Serikali ya Kenya itaendeleza ushirikiano wake na  Tanzania katika masuala ya ulinzi na usalama kwa kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Na kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi amesema Kenya na Tanzania ni ndugu tokea ezi na enzi, hivyo Serikali Tanzania itahakikisha kuwa inaendelea kushirikiana na Kenya ili kufanya ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages