July 10, 2019

Mwenyikiti w Bodi VETA aitaka Menejimenti ya VETA kupeleka bidhaa kwa wakulima.

Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Peter Maduki akipata maelezo katika banda la VETA wakati akiangalia ubunifu wa mashine mbalimbali.

Na Janeth Jovin 

Mwenyikiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Peter Maduki ameitaka Menejimenti ya VETA kupeleka  bidhaa mbalimbali kwa wakulima na isiwe kuonekana katika maonesho tu.

Maduki ameyesema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Anasema kuwa VETA imekuwa na ubunifu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kuwatambua wabunifu wa VETA.

Anasema kuwa katika kwenda katika uchumi wa Viwanda ni kazi kwetu VETA kupeleka bidhaa kwa wakulima.

Anasema kuwa Menejimenti ya VETA  iendelee kubuni bidhaa mbalimbali na kupeleka kutatua changamoto ya wananchi.
Kufika uchumi wa Kati na uchumi viwanda.

Aidha anasema kuwa bidhaa VETA ni bora kuliko zile za kutoka nje hivyo wananchi wawe na uzalendo wa kutumia bidhaa hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages