July 10, 2019

Tanzania, uholanzi wasaini randama kuinua sekta za mifuko na uvuvi

Naibu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi Bi. Marjolijn Sonnema (kushoto) akitiliana saini randama ya makubaliano na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzani, Abdalah Ulega, yaliyolenga kukuza sekta ya uvuvi na ufugaji wa kuku nchini ili kuongeza tija ya uzalishaji na kukuza sekta ya viwanda. Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Arusha.

Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi Bi.Marjolijn Sonnema (kushoto) akipeana mkono na  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzani, Abdalah Ulega (kulia) mara baada ya kuliana saini randama ya makubalinao kukuza sekta ya uvuvi na ufugaji wa kuku nchini ili kuongeza tija ya uzalishaji na kukuza sekta ya viwanda. Makubaliano hayo yamefanyika jijini Arusha. wapili kushoto ni Balozi wa Uholanzi  nchini Tanzania
Joroen Verheul na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.
  
 
Na Mwandishi Wetu, Arusha

SERIKALI ya Tanzania na Uholanzi zimesaini randama ya makubaliano ya miaka tano ya kusaidia kuinua maendeleo na ukuaji wa sekta za mifugo na uvuvi hapa nchini.

Katika makubaliano hayo yenye lengo la kuona sekta za ufugaji kuku na ufugaji wa samaki zinapata mwamko stahiki kwenye mifugo na uvuvi kwa kuwajengea uwezo watanzania wa kujikita katika uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza muda mfupi mara baada ya kuweka saini ya makubaliano hayo leo Jijini hapa, Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Bi. Marjolijn Sonnema alisema mpango huo kupitia maofisa ugani nchini nzima wataisaidia kufanisha mpango huo.

“Wafugaji watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kunufaika na mradi huuambao utaongeza uzalishaji wa chakula na biashara,” alisema waziri huyo na kupongeza makubaliano hayo yaliyofikiwa.

Kwa mujibu wa Bi. Sonnema, makubaliano hayo ya miaka mitano yatatekezwa kwa ubia kati ya sekta za umma na binafsi kwa kuvutia zaidi makampuni binafsi kutoka nchi hizi mbili yaani Tanzania na

Uholanzi. “Wataalamu watawafundisha wakulima namna bora ya kuboresha ufugaji wa kuku na ufugaji wa kisasa wa samaki katika sekta hizi mbili za mifugo na uvuvi,” alisema na kuongeza kuwa makubaliano hayo yanaendeleza mahusiano mazuri ya muda mrefu baina ya nchini hizi mbili.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bw. Abdallah Ulega alisema mkataba huo una maana kubwa kwa Tanzania kama nchi kwani utaongeza uzalishaji na kuinua maisha ya mfugaji.

“Makubaliano haya yanalenga kuhamasisha ulaji wa samaki na kuku ambao upo chini sana miongoni mwa wa Tanzania wengi,” alisema naibu waziri Ulega. Bw. Ulaga alisema Tanzania inavuna kiasi cha tani 350,000 za samaki

kwa mwaka ukilinganisha na mahitaji halisi ya tani 700,000 kwa mwaka. “Kwa takwimu hizi zinaonyesha kuwa ni kiasi kidogo sana virutubisho tunachotoa kwa kutoka na kuku na samaki,” alisema.

Naibu waziri huyo alisema kuwa bado kuna dhana potofu miongoni mwa watanzania wengi kuwa ulaji wa samaki bado ni kitu cha hanasa na siyo kwaajili ya virutubisho mwilini.

Utiliaji saini wa makubaliano hayo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maofisa waandamizi kutoka sekta za mifuko na uvuvi.

No comments:

Post a Comment

Pages