Na Suleiman Msuya, , aliyekuwa Morogoro
VIJIJI vinavyotekeleza Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, mkoa wa Morogoro, vimeshauriwa kuwa na mtaalamu mmoja kutoka Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita), ili kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu.
Ushauri huo umetolewa na Ofisa Biadhara wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ta Asili Tanzania (TFCG) Hamza Nkumulwa wakati akiwasilisha mada kwa madiwani 41 na maofisa wa idara mbalimbali za halmashauri hiyo zinazohusiana na rasilimali misitu na maliasili.
Alisema Mradi wa TTCS awamu ya pili unatarajiwa kumakizika mwezi Novemba mwaka huu hivyo ni vema halmashauri kwa kushirikiana na vijiji husika kuanza kujipanga kwa usimamizi.
Alisema vijiji vitano vya Mlilingwa, Matuli, Diguzi, Lulongwe na Tununguo ambacho hakijaanza kuvuna rasilimali misitu vinahitaji usimamizi wa wataalam kutoka Mjumita ambapo vitapaswa kutenga asilimia 7 ya mapato yake.
"Tumewasilisha mapendekezo haya ya kuwepo kwa makubaliano kuhusu utoaji huduma zinazohusu shughuli za usimamizi endelevu wa biashara za mazao ya misitu katika vijiji hali ambayo itachangia uendelevu wa misitu na uvunaji," alisema.
Nkumulwa alisema vijiji vimeanza kunufaika na mradi wa mkaa endelevu hivyo iwapo vitatoa asilimia ya mapato game kuwawezesha wasimamizi kusaidiana na wataalam wa halmashauri.
Ofisa huyo alisema makubaliano hayo yatasimamiwa na mkurugenzi ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika.
Alisema wameamua kuja na mpango huo ili kuhakikisha kila upande unakuwa salama na kwamba iwapo vijiji vitakataa wao watakuwa wametimiza wajibu wao katika usimamizi.
Akizungumzia makubaliano hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ngerengere, Kibena Kingo alisema mpango huo ni mzuri ila amewataka wataalam wa halmashauri kushirikiana na wataalam wa TFCG kwenda vijijini kuwasikiliza wanavijiji waliopo kwenye mradi.
Mwenyekiti huyo alisema iwapo wanavijiji vya vijiji vya mradi wararidhia wao kama baraza la watapitisha kwa kuwa wamepata uelewa wa nini kinahitajika.
Diwani wa kata ya Kolelo, Eridius Mbena alisema mpango huo ni mzuri ila ni vema makubaliano hayo yazingatie misingi ya kisheria kwa pande zote.
Alisema asilimia 7 ya malipo ya mtaalam wa Mjumita yabatakiwa yaoneshe ni namna gani mtaalam huyo atawajibika akikengeuka.
Mbena alisema angependa vijiji vinavyonufaika na mradi viwe na mkataba utakaowabana.
"Mradi huu umetoa matokeo chanya hivyo wananchi wanauunga mkono na ni dhahiri kuwa vijiji vingine vimeshawishika kushiriki iwapo vitapata ufadhili. Na ndio maana naomba Mjumita ijipanue zaidi kwa vijiji visivyo na mradi," alisema.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Konde, Clara Laurence alisema mradi huo umefanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi, kijamii na maendeleo hivyo wazo la mpango wa makubaliano ni nzuri na linahitajika kuungwa mkono.
"Sina mengi ya kusema ila naunga mkono mpango wa makubaliano kwani unataka kusaidia vijiji vyote vya mradi," alisema.
Meneja mradi wa TTCS, Charles Leonard, alisema mradi huo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu umefanikiwa kukusanya mapato zaidi ya shilingi milioni 800 hivyo ni jukumu la wanufaika kuangalia njia ya kuendeleza pale mradi unavyofikia ukomo.

No comments:
Post a Comment