July 21, 2019

WAZIRI NDALICHAKO ATAKA USIMAMIZI THABITI UDAHILI WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. James Mdoe, alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kufunga Maonesho ya 14 ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Karibu.
 Kutembelea mabanda ya taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu UDOM, Isidory Michael, akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu mfumo wa kuzalisha umeme kwa kutumia kishindo cha binadamu.
Waziri akipata maelezo kutoka kwa mhadhiri wa Chuo cha DIT).
Wageni.
Brass Band ikitumbuiza katika maonesho ya 14 ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa, akizungumza katika hafla hiyo.
Washiriki wa maonesho hayo wakimsikiliza waziri wa elimu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini (TURDACO), Prof. Uswege Minga, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya taasisi zilizoshiriki maonesho hayo.
Meza Kuu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Prof. James Mdoe, akizungumza wakati wa kufunga Manonesho ya 14 ya Elimu Juu, Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia na katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Amos Nungu, wakati wa kufunga Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaa.
Picha ya pamoja.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao.
 


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa wito kwa Viongozi wa Elimu ya juu nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/20 ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wanafunzi, wazazi, walezi na wafadhili wa wanafunzi hao.

Waziri Ndalichako ametoa wito huo Jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho ya 14 ya elimu ya juu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi ambayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo Jukumu la Taasisi za Elimu ya Juu Katika Kuzalisha Ujuzi Unaohitajika kwa ajili ya Viwanda.

Katika hotuba yake amesema asingependa kuona changamoto zilizotokea mwaka jana katika kujiunga na vyuo zinajirudia kwani changamoto nyingine zilisababishwa na Vyuo vyenyewe kutokuwa na mifumo thabiti ambayo wanafunzi wangeweza kufanya maombi na kujithibitisha katika vyuo kwa urahisi.

“Nafahamu kwamba TCU wameshatoa mafunzo na maelekezo ya kutosha kwa wataalamu wa mifumo ya kompyuta na maafisa udahili wa vyuo vyote ambao mnadahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2019/20 kwa hiyo naamini kwamba zoezi la udahili kwa mwaka huu litafanyika kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka jana,” alisema Waziri Ndalichako

Waziri Ndalichako  alisistiza kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu sura ya 346 ya sheria za Tanzania jukumu la kudahili wanafunzi ni la Seneti za Vyuo Vikuu au Bodi ya za Chuo husika, hivyo amewataka Viongozi wa Vyuo kutumia mamlaka ya Seneti za Vyuo Vikuu au Bodi kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu udahili wa wanafunzi ili waweze kujiunga kwa urahisi huku akisistiza pia  vigezo, masharti, taratibu na sifa za mwanafunzi kujiunga na chuo kuzingatiwa.

“Niwakumbushe tu  Serikali iko macho, katika mchakato wa udahili msipofuata taratibu mkaweka watu wasio kuwa na sifa tutawaondoa lakini kumbukeni na ninyi mloiwaingiza hamtabaki salama, hakikisheni zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi,”aliongeza Waziri Ndalichako.

Sambamba na hilo amewataka wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu kutokuwa wavivu wa kusoma maelekezo kabla ya kuanza kujiunga ama  kuchagua kozi katika vyuo. Amewaasa kuzingatia sifa zinazohitajika kwa kulinganisha ufaulu wao wakati wa kuchagua kozi huku akisistiza kuwa Serikali haina utaratibu wa kumpangia mwanafunzi programu ya kusoma isipokuwa inachagua mwanafunzi kutokana na sifa alizonazo katika kozi husika.

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu ya juu na Vyuo vikuu kuendelea kujitathmini ni kwa kiasi gani  tafiti ambazo wamekuwa wakizifanya zinagusa moja kwa moja jamii na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali  zilizopo katika jamii.

“Ninyi Taasisi za Elimu ya Juu macho yenu na masikio yawe wazi kila mara ili muweze kusikiliza wapi katiika jamii kuna changamoto na kwa kutumia utaalamu wenu mshiriki kuzitatua, kumbukeni elimu ya juu katika nchi yoyote ile ndio kitovu cha maarifa hivyo muendelee kutumika katika kutatua changamoto hizo,” aliongeza waziri Ndalichako.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa maonesho Profesa Uswegi Minga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Tumaini amesema uwepo wa maonesho hayo umetoa nafasi ya vyuo vyenyewe kujitangaza kuhusu fursa zinazopatikana katika vyuo vyao, lakini pia imekuwa nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu  kutokana na kujifunza namna vyuo vingine vinavyofanya kazi hivyo kusaidia kufanya maboresho katika maeneo ya uendeshaji wa Vyuo lakini pia katika upangaji na ufundishaji wa programu mbalimbali.

Maonesho hayo ya 14 ya Vyuo vya Elimu ya Juu yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini na kwa mwaka huu yamekuwa na washiri zaidi ya 80 vikiwemo kutoka nje ya nchi na vile vyaTanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages