August 06, 2019

TCRA yawataka Wananchi waliopata changamoto ya mawasiliano kwenda Maonesho kupata ufumbuzi

 Wanafunzi  na Wananchi wakipata wakipata maelezo katika banda la TCRA katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini mkoani Arusha.
Wananchi wakipata huduma katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini mkoani Arusha.
 Wanafunzi wakipata elimu ya mawasiliano katika banda la TCRA katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini mkoani Arusha.
 Afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Noah Lalataika akimpa maelezo huduma mwananchi aliyetembelea Banda la TCRA katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha.


Na Mwandishi Wetu

 Wananchi wa mkoa wa Arusha na maeneo  ya jirani  wamehimizwa kutumia fursa ya maonyesho  ya 88 yanayoendelea kusajili upya namba zao za simu na kuthibitisha kwa njia ya kibiometria kwani huduma hiyo inapatikana katika  maonyesho pamoja na waliopata changamoto ya mawasiliano kwenda katika kupata ufumbuzi.

Akizungumza katika  Banda la maonyesho  la Mamlaka ya Mawasiliano  (TCRA) kanda ya Kaskazini  Mkuu wa kanda Hiyo  Mhandisi  Imelda Salum amesema TCRA ikishirikiana  na makampuni ya simu  wamehakikisha kuwa huduma hiyo  inakuwepo  kurahisisha na kusogeza huduma kwa wananchi.

Amesema sambamba na huduma hiyo TCRA pia inatoa elimu  ya matumizi  bora na salama ya huduma za mawasiliano  na kuwataka wananchi wenye matatizo  wafike bandani  hapo kwa ajili ya ushauri

No comments:

Post a Comment

Pages