August 03, 2019

WANANCHI SINGIDA WATAKIWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MBUNGE WAO

 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akivikwa shada la maua baada ya kuwasili Kijiji cha Kitandaa kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara wilayani Ikungi mkoani Singida jana. Mbunge Kingu alifanya mikutano miwili katika kijiji hicho na makao makuu ya Kata ya Mtunduru.
 Wakina mama wa Kijiji cha Kitandaa wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea Kijiji cha Kitandaa.
 Mbunge Kingu akisalimiana na wazee wa Kata ya Mtunduru baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya mkutano.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzì (UVCCM) wilaya ya Ikungi, Jafari Dude akizungumza kwenye mkutano huo.
 Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Ikungi, Himid Tweve, akiimbisha wimbo wa viongozi wamechachamaa.
 Diwani wa Kata ya Mtunduru Ramadhan Mpakii akizungumza.
 Wanawake wa Kata ya Mtunduru wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mbunge Kingu akihutubia kwenye mkutano huo wa Kata ya Mtunduru.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale, Singida

DIWANI wa Kata ya Mtunduru katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Ramadhani Mpakii amesema jitihada zinazofanywa na Mbunge wao Elibariki Kingu za kuwapelekea miradi ya maendeleo zinapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo wa Jimbo la Singida Magharibi.

Akizungumza kwa nyakati tofauti jana kwenye mikutano ya hadhara aliyoandaa mbunge huyo katika vijiji vya Kitandaa na Mtunduru Mpakii alisema haijawahi kutokea tangu vianzishwe vijiji hivyo kwa kupata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka minne tangu mbunge huyo aingie madarakani.

" Mbunge huyu hana wa kumlinganisha naye ni msikivu na amejitahidi sana kutuletea maendeleo katika Kata yetu ebu tumuache aendelee kututumikia kwa kipindi kingine kwanza umri wake bado ni mdogo " alisema Mpakii.

Alisema katika kata hiyo ameweza kujenga shule, zahanati, na sasa amewaletea mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh.milioni 405 ambao utasambaza maji kwenye vijiji vyote vya kata hiyo.

Mpakii aliongeza kuwa tangu miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea Mbunge kama Kingu kwani kazi iliyofanywa na Rais Dkt.John Magufuli na Mbunge huyo ya kuwapelekea miradi hiyo itawarahisishia upatikanaji wa kupata kura nyingi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mtaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

" Kwa kazi hii kubwa iliyofanyika hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi kuufanya" alisema Mpakii.

Akizungumza katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi na kuwaambia maendeleo hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kwa wananchi wanyonge kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.

Alisema haijawahi kutokea kwa kipindi chote kilicho pita ndani ya jimbo hilo kufanyika kwa miradi mingi kiasi hicho ikiwemo miradi mikubwa ya maji 24 huku mchakato wa kupata umeme wa REA ukiendelea na kuwa amepata fedha zaidi ya sh. milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Sekondari ya Mtunduru.

Wakati huo huo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji, ametoa onyo kwa wanachama wa chama hicho kuanza kujipenyeza kwenye majimbo ili kuwania nafasi za ubunge na udiwani wakati majimbo hayo yakiwa na wawakilishi.

No comments:

Post a Comment

Pages