Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dk. Naftali Ng’ondi.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) chini ya uratibu wa Kamishina
wa
Ustawi wa Jamii imeunda timu maalum ya wataalam wa Ustawi na Maendeleo
ya Jamii
kwa ajili ya kufanya tathmini ya athari na mahitaji yanayotokana na
janga la moto mkoani Morogoro pamoja na kutoa huduma ya msaada wa
Kisaikolojia na Kijamii na kuwaunganisha
wahitaji na huduma mbalimbali.
Hayo yamesemwa mkoani Morogoro na Kamishna wa
Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi wakati alipofika katika maeneo mbalimbali
kuzungumza na ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali
hiyo.
Kamishna
Ng'ondi amesema kuwa katika zoezi hilo Wizara
inashirikiana na wataalam kutoka ngazi ya Mkoa, Halmashauri na wataalam
kutoka Chama cha wataalam wa Ustawi wa Jamii (TASWO), Taasisi ya Ustawi
wa Jamii na Chuo
Kikuu cha Dar es salaam.
Kamishna Ng'ondi ameongeza kuwa Wataalam hao pamoja na
kutoa msaada wa kisakolojia na kijamii pia watafanya kazi ya kutambua watoto
walio katika mazingira hatarishi kutokana na kupoteza wazazi/walezi na kuainisha
mahitaji yao, kuwasajili, na kuwaunganisha na huduma kwa kushirikiana na
viongozi husika.
Amezitaja huduma nyingine zitakazotolewa na
wataalam hao kuwa ni kutoa huduma ya Msaada wa Kisaikolojia na kijamii kwa
watoa huduma Hospitalini, kuzuia matatizo zaidi ya kimwili, Kiroho na kiakili,
na kujumuisha hatua za matibabu kwa waathirika, ikiwa ni pamoja na aina
mbalimbali za ushauri, kama vile ushauri wa huzuni (Bereavement Counseling) baada
ya ajali na kuunganisha wagonjwa kwa wataalamu na vituo vya matibabu.
Kamishna Ng’ondi ameeleza kuwa Idara ya Ustawi wa
Jamii na Maendeleo ya jamii zitasaidia pia kuwaunganisha wahanga na programu za
kijamii (Wahudumu wa Mashauri ya Kijamii – Community Case Workers, Para Social
Workers) zitakazowasaidia watoto kuondokana na hali ya majonzi na kuwaunganisha
na huduma za kijamii kulingana na mahitaji na upatikanaji wa huduma na
rasilimali zilizopo zikiwemo Hospitali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, asasi za
kiraia na watoa huduma binafsi.
Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wataalam kutoka Mkoa
wa Morogoro wanaandaa jumbe mbalimbali kwa ajili ya kuelemisha jamii kuhusu ulinzi
na usalama kwa jamii na jinsi ya kukabiliana na majanga ili kuepukana na
majanga yanayoweza kuepukika.
Ajali ya Lori la mafuta
lililolipuka eneo la Msamvu mjini Morogoro, Jumamosi tarehe 10/08/2019 saa
mbili asubuhi limesababisha vifo zaidi ya watu 70 na majeruhi
zaidi ya 40 waliungua kwa moto baada ya lori lililokuwa na shehena ya mafuta
kupata ajali na kisha kupinduka na kulipuka moto.
No comments:
Post a Comment