HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 15, 2019

RAIS CYRIL RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI

 Rais Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es Salaam usiku huu. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC.
 Rais Cyril Ramaphosa akipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es Salaam usiku huu. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika SADC.
Rais Cyril Ramaphosa akipeana mikono  na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es Salaam usiku huu. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, Mkuu wa Wiklaya ya Kigamboni Mhe. Mhe. Sarah Misafiri na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC.
 Rais Cyril Ramaphosa akipeana mikono  na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni Kamanda wa Kanda Mazlumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam Lazaro
Mambosasa. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC.


 Rais Cyril Ramaphosa akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es Salaam usiku huu. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanacha. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages