Balozi Mteule wa
Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo
Fanti akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akiongea na Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Meja
Jenerali Karamba Charles jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Itifiki wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge
akimkaribisha Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Meja
Jenerali Karamba Charles katika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea hati ya
utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea hati ya
utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Rwanda
nchini, Meja Jenerali Karamba Charles.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika picha ya pamoja na
Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti na Mkuu wa Itifiki wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge, pamoja Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba
Charles. Kulia ni Mkuu wa Itifiki wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti.
Mazungumzo hayo yamefanyika
jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Balozi Fanti kuwa Uhusiano
kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ni wa Muda mrefu tangu mwaka 1975 ambao hadi
sasa Tanzania imekuwa na mahusiano imara na umoja huo.
"Ushirikiano
wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umelenga kupunguza umasikini, kukuza maendeleo
endelevu, na kusaidia ujumuishaji wa Tanzania katika uchumi wa dunia, mpango
kazi wa ushirikiano huu unaundwa na nguzo kuu tatu ambazo ni maendeleo ya
uchumi, biashara na uwekezaji pamoja na mazungumzo ya kisiasa. Msaada wa Umoja
wa Ulaya umeweza kushughulikia changamoto mbalimbali katika ajenda za maendeleo
ya kitaifa" Alisema Prof. Kabudi
Waziri
Kabudi ameongeza kuwa, kulingana na takwimu za mwaka 2017, Umoja wa Ulaya unaonekana
ndiye mshirika mkubwa zaidi wa biashara ya bidhaa kwa Tanzania baada ya India, kwa
asilimia 13.1. Bidhaa zinazoingizwa kutoka Umoja wa Ulaya ni pamoja na mashine,
vifaa, bidhaa za kemikali na vifaa vya usafirishaji.
Prof.
Kabudi amegusia pia mazungumzo ya kisiasa na kueleza kuwa ni nguzo muhimu ya
uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya. Mazungumzo ya kisiasa yanalenga kuongeza
uwazi na umoja ili kukuza uelewa wa pamoja katika vyama vya siasa.
Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,
Balozi Manfredo Fanti amesema kuwa Umoja huo upo tayari kusaidia Tanzania na
kuhakikisha kuwa sera za nchi zinasonga mbele ili kuiwezesha Tanzania kuwa na maendeleo endelevu na kusaidia malengo ya nchi.
"Pia tupo tayari kuhakikisha kuwa
uwekezaji na biashara unaofanywa kati ya Umoja wa Ulaya pamoja na Tanzania
unakuwa wa manufaa kwa pande zote lengo likiwa ni kukuza sekta ya biashara hapa
Tanzania" Balozi Fanti.
Katika
tukio jingine Waziri wa Mamno ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini, Meja Jenerali Karamba
Charles ambaye ameelezea uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Rwanda
ni wa kiwango cha juu na kuongeza kuwa jukumu lake kubwa kwa sasa ni kuongeza
kiwango cha biashara na uswekezaji kati ya Nchi hizo mbili.
Meja
Jenerali Karamba Charles ameyasema hayo wakati akikabidhi nakala za hati ya
utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) kuchukua nafasi ya aliyekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania
Balozi Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake.
No comments:
Post a Comment