HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 18, 2019

Wanataalam 250 wa sayansi, teknolojia, ubunifu kukutana Dar

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa wanataaluma ya sayansi, teknolojia na ubunifu utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 11 hadi 15 mwaka huu.



Na Suleiman Msuya

WANATAALUMA wa Sayansi, Technolojia na Ubunifu 250 wanatarajiwa kukutana  jijini Dar es Salaam katika mkutano wa viongozi wa kikanda wa baraza la Sayansi kanda ya Afrika.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 11 hadi 15 mwaka huu umeandaliwa na Tume ya Sayansi na Technolojia Tanzania (COSTECH).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Kaimu Meneja wa Utafiti wa Sayansi hai wa COSTECH, Dk. Hulda Gideon, amesema  mkutano  huo wa wanataaluma utatoa nafasi pana ya kujadili masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

Alisema mkutano huu utahusisha wadau wa sayansi, technolojia na ubunifu, wanasayansi, wafadhili, watunga sera washirika wa Maendeleo pamoja na wanahabari.

"Mada kuu katika mkutano huo ni Uwazi wa Sayansi kwa Maendeleo Endelevu na Ushirika wa Umma katika masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu," amesema.

Amesema mkutano huo wa viongozi wa kikanda utaambatana na maonesho ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU).

Dk. Hulda amesema kuwa Mada zitkazotolewa katika mkutano huo zitaaaidia kutayarisha ajenda za mkutano wa baraza la dunia utakaofanyika Afrika ya kusini 2020.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu amewaomba wadau wa STI na umma kwa ujumla kutambua uwepo wa mkutano huo wa viongozi wa juu wa Sayansi wa Afrika.

Nungu amesema kuwa Mkutano huo utafunguliwa na waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako Novemba 11 mwaka huu

No comments:

Post a Comment

Pages