HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 18, 2019

BOND FUND YA UTT AMIS YAREJEA TENA SOKONI

Na Mwandishi Wetu
BAADA ya zuio la mwezi mmoja Mfuko wa uwekezaji wa ‘Bond Fund’ unaoendeshwa na Kapuni ya UTT AMIS umerejea sokono kwa wateja kupata fursa ya kununua vipande vya hati fungani kuanzia Novemba 16 mwaka huu.
UTT AMIS inasimamia takribani mifuko mitano ya uwekezaji ambayo ni Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Jikimu na Ukwasi na sasa mfuko wa sita ni ‘Bond Fund’ wenye lengo la kutoa gawio, kulingana na faida itakayopatikana pamoja na kukuza mtaji kwa wawekezaji wa muda mrefu.
Akizindua awamu ya pili ya mauzo ya vipande vya mfuko wa Bond, Mkurugenzi Mkuu wa UTT AMIS, Simon Migangala amesema mauzo ya awamu ya kwanza yalikuwa mazuri, kwa ushiriki wa wawekezaji karibia 2000, huku kiasi kilichokusanywa ni Tsh, Bilioni 15.9.
“Mifuko ya uwekezaji wa pamoja huwa ina mauzo ya awali halafu baada ya kipindi cha mwezi mmoja huwa tunafungua tena, tukisha fungua sasa yanakuwa ni mauzo endelevu, awali tulifungua Septemba 16, mauzo yakaenda hadi Oktoba 15.
“Mauzo yalienda vizuri sana, wawekezaji wengi walijitokeza  karibia 2000 walishiriki kununua vipande vya mfuko wa ‘Bond Fund’ na kiasi ambacho kimekusanywa katika kipindi hicho TSh, Bilioni 15.9, Wawekezaji tunawashukuru wameweza kuitikia wito kwa kiasi kikubwa sana.
“Kuanzia Novemba 16, kulingana na ruhusa ambayo tumepewa na masoko ya mitaji na dhamana, tunafungua mauzo tena, kwaiyo kwa wawekezaji ambao walikosa nafasi ya kununua vipande vya mfuko wa ‘Bond Fund’ hapo awali sasa wananafasi ya kuweza kufanya hivyo.”amesema Migangala.
“Baada ya mauzo ya awali kufungwa mwezi oktoba kuna wateja ambao waliendelea kuwekeza, kuna maswali fedha zao zitafanywaje?, Ni kwamba vipande vyao vitagawiwa kwa kutumia thamani ya bei ya kipande ya awamu hii ya pili ya kuanzia Novemba 16.
“Pia tunawawekezaji karibia 2000 ambao walifungua akaunti, 1415 wao waliweka pesa katika kipindi cha mwezi wa mwanzo, lakini kuna wawekezaji 551 wao hawakuweza kuweka pesa, kwaiyo sasa hivi ni fursa kwao kuwekeza katika mfuko kupitia zile akaunti zao kwani bado ziko hai.”amesema Issa Wahichinenda, Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa UTT AMIS.
Nae Mkurugenzi wa Tehama wa Kampuni hiyo, Sophia Mgaya amesema UTT AMIS, imeendelea kurahisisha huduma kwa wawekezaji wao kupitia njia za Simu na Mitandao ya kijamii.
“Kwa sasa UTT AMIS huduma zetu zinapatikana kiganjani kwa maana njia za simu, unaweza kupata huduma hizi za kununua vipande, kufungua akaunti ama kupata taarifa ya uwekezaji wako kupitia huduma ya *150*82# ama kwa kupakua ‘App’ yetu ya UTT AMIS, lakini pia tumejiunganisha na mitandao ya simu, hata bila kuwa na App yetu unaweza kununua vipande kupitia T-Pesa, M-Pesa, Airtel Money na T-Pesa.
“Lakini pia tumeunganisha mfumo wetu na Benki ya CRDB kwa wateja wote wa CRDB wanaweza kununua vipande kwa kupitia akaunti zao za benki ya CRDB wanazotumia.”amesema Mgaya.
Katika hatua nyingine Mifuko mingine ya UTT AMIS ukiondoa ‘Bond Fund’ itafanya mikutanao ya mwaka Novemba 30 na Desemba Mosi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages