HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2019

MWAKINYO AMTWANGA MFILIPINO KWA POINTI

HASSAN Mwakinyo bondia wa ngumi za kulipwa Tanzania  amemtwanga mpizani wake kwa pointi ushindi ambao haujamfurahisha dhidi ya Arnel Tinampay.

Kwenye pambano la raundi 10 lililopigwa uwanja wa Uhuru, Mwakinyo alishinda kwa pointi jambo ambalo hajafurahia.

"Sijafurahia aina ya ushindi niliuupata ila ni sehemu ya matokeo kwa kuwa ushindani ulikuwa mkubwa na gloves hazikuwa rafiki kwangu, wakati mwingine nitakuwa tofauti zaidi ya hapa," amesema Mwakinyo.

Matokeo ya jumla yapo namna hii:-Jaji wa kwanza ametoa 97 -93 , Jaji wa pili akatoa 98-92 na Jaji wa tatu akatoa 96-96.



No comments:

Post a Comment

Pages