HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2019

SIMBA YAMTUPIA VIRAGO KOCHA WAO

HATIMAYE kibuyu kimelia huko Msimbazi, Uongozi wa klabu ya Simba umevunja mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu klabu ya Simba kwa madai ya utovu wa nidhamu. 

Simba wamefikia hatua hiyo ikiwa ni baada ya taarifa za kufukuzwa mbelegiji huyo kushika kasi kwa muda sasa. 

Aussems ameitumikia Simba kwa misimu miwili na robo na kufanikiwa kuwapatia Makombe mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara VPL,  Ngao ya jamii na kufanikiwa kuifikisha hatua ya Robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL msimu uliopita. 

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu Auseems amefukuzwa kwa utovu   wa nidhamu kushindwa kuheshimu sehemu ya kazi na kuondoka kituo cha kazi bila taarifa. 

Kwa sasa aliyekuwa msaidizi wake Denis Kitambi atakaimu nafasi yake huku Uongozi kufanya jitihada za dhati kumpata Kocha Mkuu.

No comments:

Post a Comment

Pages