Baadhi ya
Wachezaji kutoka Vilabu Mbalimbali wakiwa tayari kwa ajili ya kuingia katika
Mchuano wa mashindo ya Wazi ya Tanzania open katika Uewanja wa Kili jijini
Arusha.
Naibu
Waziri wa mambo ya Nje Damas Ndumbaro (katikati) akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi
wa Chama cha Gofu Tanznaia (TGU) kabla ya kuingia Uwanjani katika mashindano
hayo yaliyochukua Siku Tatu .
SELEMANI SEMUNYU
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Damas Ndumbaro, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika
ufungaji wa mashindano ya wazi ya Gofu ya Tanzania open yanayofanyika katika
Uwanja wa Kili Jijini Arusha.
Akizungumza
katika Siku ya Pili ya Mchezo huo
Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Criss Martin alisema
Maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni hitimisho kesho Jumapili licha ya mvua iliyonyesha Nyakati za mchana.
“ Mvua
ilinyesha lakini bahati nzuri haijaathiri kiasi cha kuvunja mchezo licha ya kuchelewesha
wachezaji ambao iliwalazimu kujificja kwa ajili ya Mvua na muda kwenda lakini
hali ikawa sawa “ Alisema Mwenyekiti wa TGU.
Aidha
alisema anawashukuru wadau wote waliofanikisha mashindano haya makubwa wakiwemo
Verge Africa ambao wamehakikisha maandalizi yote yamekamilika ikiwemo
upatikanaji wa Wadhamini ambao ndi mafanikio ya mashindano.
Kwa upande
wake Mchezaji Victor Joseph ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya tanznai
kwa kuongoza katika wachezaji wa Divisheni A baada ya kupiga 71 nna kuendelea
kuongoza na kubakiza matumaini ya Watanzania.
Victor alisema
licha ya Mvua lakini bado anaendelea kupambana kuhakikisha kikombe kinabaki
Tanznaia kutokana na uwepo wa wachezaji kutoka nchi Nyingine amabao wameshiriki
katika Mashindano haya.
Kwa Upande
wa Wachezaji wa Kulipwa kutoka Kenya
Dismass Indiza ameendelea kuongoza huku kwa Wachezaji wa Ridhaa Victor
joseph wa klabu ya Golf ya Dar es Salaam
Gymkhana wameendelea kufanya vyema.
Kwa upande
wake Dismass Indiza alisema mchezo umekuwa mgumu siku ya pili baada ya siku ya
kwanza kutokana na mvua na hata ushindani haukuwa wa nguvu kufuatia hali ya
hewa lakini matumaini yake yake katika hatua ya mwisho ya fainali Desemba 1, 2019.
No comments:
Post a Comment