Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, akimtunuku Shahada ya Mipango na Usimamizi wa Mazingira mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, katika Mahafali ya 33 ya chuo hicho. (Picha na Farida Ramadhani-Wizara ya Fedha na Mipango).
Benny Mwaipaja, Dodoma
NAIBU Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, amekitaka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,
kutafiti kwa kina namna wananchi wanavyoweza kuondokana na umasikini wa kipato
pamoja namna Miradi mbalimbali ya Serikali inavyoweza kutekelezwa kwa ufanisi
na kwa kuzingatia thamani ya fedha kuliko ilivyo sasa.
Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo
wakati akiwatunuku astashahada na shahada mbalimbali wahitimu 3,182 Wa Chuo cha
Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi ya Dodoma wakati wa sherehe za mahafali
ya 33 ya chuo hicho.
Amesema kuwa matokeo ya
tafiti hizo yataisaidia Serikali na Jamii kwa ujumla kupanga mikakati ya namna
ya kukabiliana na umasikini wa wananchi hususan wa vijijini pamoja na
kuharakisha maendeleo ya nchi kwa kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa na
Serikali inakuwa na tija.
Kwa upande wake Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa
Bajeti Bw. Pius Mponzi amemwahidi Dkt. Ashatu Kijaji, kwaniaba ya Baraza la
Chuo hicho kwamba wataongeza jitihada katika eneo la utafiti na kuhakikisha
kuwa matokeo ya utafiti huo yanawafikia wananchi kwa lugha rahisi.
Naye Mkuu wa Chuo hicho cha
Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya amesema chuo chake
kimetimiza miaka 40 tangu kianzishwe na kimepata mafanikio makubwa kwa kutoa
wahitimu mahili na wenye kukidhi mahitaji ya soko.
Amebainisha kuwa Chuo
kimeongeza idadi ya kozi kutoka kozi moja mwaka 1980 hadi kufikia kozi 25 mwaka
huu, huku idadi ya wanachuo wanaodahiliwa nayo imeongezeka kutoka wanachuo 13 mwaka
huo hadi kufikia wanachuo zaidi ya elfu 11 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment