November 27, 2019

Nancy Sumari azindua kitabu cha Haki ya mtoto

Nancy Sumari.

 Na Janeth Jovin

WAZAZI, walezi  na jamii kwa ujumla wametakiwa kutambua kuwa wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi ikiwamo ya kupata elimu, chakula, afya bora, kucheza pamoja na usalama wao wa kuishi.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo na mwandishi wa kitabu cha Haki Nancy Sumari wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kitabu hicho.

Sumari alisema anafahamu kuwa sheria na hazi za watoto zipo lakini walio wengi awazifahamu hivyo ipo haja ya jamii kuzifahamu kwa kina na kuhakikisha wanazifuata ili kuweza kuwa na kizazi bora cha sasa na baadae.

"Nimeandika kitabu hiki kwanza kuwasaidia watoto watambue haki zao ili waweze kuzisimamia na wasinyanyaswe  wala kufanyiwa ukatili, lakini pia wazazi, walezi na jamii kwa ujumla nao wazisome na watambue wajibu wao kwa watoto.

Kitabu hiki, kimekamilika na kitauzwa kwa sh. 6000 lakini natambua kuwa wapo watoto na wazazi ambao hawana uwezo wa kununua hivyo nitakiweka katika maktaba kuu ya taifa na watakisoma bure kabisa wakienda huko," alisema.

Alisema ndani ya kitabu hicho cha Haki kuna picha nyingi ambazo zimeambatana na maneno ambayo yatawasaidia watoto kujifunza zaidi huku wazazi na walezi kusoma na kuelewa kwa urahisi haki za watoto.

Aidha alisema anaamini kuwa kitabu hicho kitawafikia watoto wengine na kuongeza kuwa malengo yao ni kuhakikisha kila mtu anapata fusra ya kukiona na kukisoma.

"Nimeandaa kitabu hiki kwa miaka minne mpaka mitano na kimeandakwa kwa lugha ya Kiswahili kwa kuwa natambua kuwa lugha hii yetu imefikia sasa hadhi ya kimataifa, hivyo nami anaendelea kukiimarisha kiswahili," alisema.

Aidha Sumari amewataka wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao wanapata muda wa kutosho wa kucheza kwani jambo hilo uwajenga zaidi kimwili na kiakili.

"Unajua wazazi wengi wanafikiria kuwa watoto wakicheza wanapoteza muda jambo ambalo si kweli hata kidogo, niwaambie kuwa watoto wanaopata muda wa kucheza wanajengeka kiakili na kimwili," alisema Sumari.

No comments:

Post a Comment

Pages