November 15, 2019

RC TABORA JITOKEZI KUSHIRIKI MARATHON YA KUTANGAZA VIVUTIO VYETU

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana kuhusu umuhimu wa wakazi wa Tabora kushiriki Tabora Green Marathon kwa ajili ya utunzaji mazingira. (Picha na Tiganya Vincent).
Mratibu wa Tabora Green Marathon  James Mackanza akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika mwishoni mwa Mwezi huu.
 

Na Tiganya Vincent
 
WAKAZI Mkoani Tabora wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Tabora Green Marathon ambazo ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha jamii ili iweze kushiriki katika usafi na utunzaji wa mazingira.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tabora Green Marathon.

Alisema mbio hizo zinalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayohimiza usafi na utunzaji wa mazingira kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mwanri alisema wakati wa mbio hizo washiriki watapanda miti katika maeneo mbalimbali na kutangaza vivutio vya utalii ambavyo vinapatikana Mkoani Tabora kwa ajili ya kuwakaribisha wawekezaji katika sekta hiyo.

Naye Mratibu wa Mashindano hayo James Mackanza alisema wao kama wakazi  waliopo Manispaa ya Tabora wameamua kuandaa mbio hizo maalumu ili kuunga mkono juhudi za Serikali za  upandaji miti na usafi wa mazingira.

Alisema mbio hizo zinatarajiwa kufanyika mwisho mwa Mwezi huu ambapo wamemuomba Mwanamziki Maarufu hapa nchini Ali Kiba kushiriki katika shughuli za kijamii mkoani Tabora siku hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Tabora kujitokeza kujiandikisha ili wapate fursa ya kushiriki na kuweka alama ya utunzaji mazingira mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Pages