Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari jana kuhusu umuhimu wa wakazi wa Tabora kushiriki Tabora Green
Marathon kwa ajili ya utunzaji mazingira. (Picha na Tiganya Vincent).
Mratibu
wa Tabora Green Marathon James Mackanza akizungumza na waandishi wa
habari jana kuhusu maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika
mwishoni mwa Mwezi huu.
Na Tiganya Vincent
WAKAZI Mkoani Tabora wametakiwa kujitokeza kwa
wingi kushiriki mbio za Tabora Green Marathon ambazo ni maalum kwa ajili ya
kuhamasisha jamii ili iweze kushiriki katika usafi na utunzaji wa mazingira.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi
ya Tabora Green Marathon.
Alisema mbio hizo zinalenga kuunga mkono
juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayohimiza usafi na utunzaji wa mazingira
kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mwanri alisema wakati wa mbio hizo washiriki
watapanda miti katika maeneo mbalimbali na kutangaza vivutio vya utalii ambavyo
vinapatikana Mkoani Tabora kwa ajili ya kuwakaribisha wawekezaji katika sekta
hiyo.
Naye Mratibu wa Mashindano hayo James Mackanza
alisema wao kama wakazi waliopo Manispaa
ya Tabora wameamua kuandaa mbio hizo maalumu ili kuunga mkono juhudi za Serikali
za upandaji miti na usafi wa mazingira.
Alisema mbio hizo zinatarajiwa kufanyika
mwisho mwa Mwezi huu ambapo wamemuomba Mwanamziki Maarufu hapa nchini Ali Kiba
kushiriki katika shughuli za kijamii mkoani Tabora siku hiyo na kutoa wito kwa
wakazi wa Tabora kujitokeza kujiandikisha ili wapate fursa ya kushiriki na
kuweka alama ya utunzaji mazingira mkoani humo.
No comments:
Post a Comment