Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mohamoud Thabiti Kombo (wa pili kushoto), akiteta jambo na Rais wa Umoja wa Kamati za Olimpiki Afrika (ANOCA), Mustapha Berraf. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau na Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, baada ya ufunguzi wa semina ya makatibu wakuu wa ANOCA. (Na Mpiga Picha Wetu).
Makatibu Wakuu wa Kamati za Olimpiki za Afrika
wakishiriki katika ufunguzi wa semina ya 36 ya Makatibu wakuu wa Umoja wa
Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA) ulioanyika katika Hotel Verde mjini
Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu Zanzibar
SEMINA ya 36 ya Makatibu Wakuu wa Umoja wa Kamati za
Olimpiki za Afrika (Anoca) imevunja rekodi baada ya nchi zote 54 za Afrika
kushiriki katika hafla hiyo iliyofanyika katika hotel ya Verde mjini hapa.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud
Thabit Kombo alisema ni jambo la kujivunia sana kwa makatibu wa nchi zote 54 za
Afrika kushiriki katika semina hiyo, ambayo ilianza jana mjini hapa.
“Kwakweli ni jambo la kujivunia sana kwa nchi zote 54
za Afrika kuhudhuria semina hii nah ii inadhihirisha kuwa Zanzibar na Tanzania
kwa ujumla ni mahali, ambako kila mtu anapenda kutembelea, “alisema Kombo,
ambaye mara kwa mara alikuwa alipigiwa makofi na wajumbe wakionesha kufurahia
hotuba yake.
Ilielezwa katika semina hiyo ikifanyikia katika nchi
zingine wamekuwa wakihudhuria makatibu wachache ukilinganisha na Zanzibar,
ambako nchi zote zimehudhuria bila kukosa.
Alisema ni heshima kubwa kwa mkutano huo kufanyikia
Zanzibar na yeye kupata nafasi ya kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina
hiyo muhimu wakati tukielekea Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 nchini Japan.
Alisema
mikutano kama hiyo inasaidia sana kuitangaza Zanzibar kiutalii,ambapo aliwataka
makatibu hao kutembelea kisiwa hicho pamoja na kile cha Pemba ili kujionea vivutio
kibao.
Pia alisema kuwa Zanzibar ni nzuri kwa mashindano ya
michezo ya ufukweni kama vile soka, mpira wa wavu na hata mchezo mpya wa
Teqball, ambao ulitambulishwa rasmi jana mjini hapa na Waziri Kombo) alipata
nafasi kuhushuhudia mchezo huo uichezwa,
Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) alisema
kuwa ni furaha kubwa kuandaa semina hiyo Zanzibar kwani pamoja na Tanzania kwa
jumla ni mahali pazuri na watu wake ni wakarimu.
Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau ndiye
aliyezungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Rais wake, Gulam Rashind, ambaye
alikuwa na shughuli nyingine ya kitaifa.
Baada ya ufunguzi huo, semina hiyo ilianza kwa
makatibu ambao nchi zao zinazungumza Kifaransa huku wale wa Kiingereza semina
yao inafanyika leo katika hoteli hiyo Verde mjjiji hapa.
Pia katika ufunguzi wa semina hiyo ulikuwepo ujumbe
wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki Tokyo 2020, Wawakilishi wa
Olimpiki Silidarity (OS) na Ujumbe kutoka Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki
(IOC).
Semina hiyo ilijadili mambo mbalimbali ikiwemo
Michezo iliyopita ya Olimpiki na nini nchi za Afrika kufanya katika michezo
ijayo ya Tokyo 2020 na mambo mengine ya michezo kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment