Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati akizungumza mbele ya
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga
wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga
akizungumza na wakazi wa Kigoma pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo
wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo Mkoani Kigoma, Kulia ni Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga
akihakiki utendaji kazi wa mfumo wa kusajili namba za simu kwa alama za
vidole katika duka jipya la Tigo lililopo eneo la Lubengela Mkoani
Kigoma jana mara baada ya kuzindua duka hilo.Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo
Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati.
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania imezindua
duka jipya mkoani Kigoma hali ambayo itawezesha
watejawa
wake kupata huduma zilizoboreshwa zaidi.
Duka
hilo jipya litakuwa sehemu maalumu kwa ajili ya wateja kujionea na kufanya
majaribio ya bidhaa na huduma mbalimbali mpya na za kidigitali kama TigoPesa
zitolewazo na kampuni hiyo.
Wateja
pia wataweza kupata huduma ya kusajili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za
vidole.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenziwa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati
alisema. “Ufunguzi wa duka hili ni
utekelezaji wa mkakati wa Tigo wakufikisha huduma karibu na wateja na tunaamini
kuwa duka hili litatoa fursa za biashara kwa wateja na kuchochea ukuaji wa
uchumi mkoani hapa,”.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliipongeza Tigo
kwa
jitihada
zake za kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye viwango vya kimataifa maeneo
yote ya nchi.
“Duka
hili jipya litakuwa chachu katika uboreshaji wa huduma za mawasiliano hapa
mkoani Kigoma. Mkoa huu una wakazi wachapa kazi na wafanyabiashara ambao
wanatamani kujikwamua kiuchumi hivyo hii ni fursa muhimu kwao,” alisema.
Aliongeza “Hii ni faraja kuona kwamba sasa huduma za
Tigo zitapatikana kwa urahisi zaidi na hii itasaidia kufungua fursa nyingi za
kiuchumi.”
Duka
hilo linapatikana katika mtaa wa Lubenge la Kigoma Mjini, ni la kwanza mkoani
humo na litakuwa likitoa huduma sambamba na dawati la wateja lililopo wilayani
Kasulu. Duka hili limewekwa katika eneo hili kimkakati ilikufikika kwa urahisi
kwa wakazi.
Duka
hilo linaifanya Tigo kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma zake maeneo
mbalimbali ya nchi ilikufikia wateja wake zaidi ya milioni 11.6 jambo
linalofungua milango kwa wateja kufurahia huduma za kidigitali zinazotolewa na
kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment