November 27, 2019

Serikali kuboresha sera, kukitangaza kilimo hai

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, akizungumza na washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Kilimo hai uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa kimataifa wa kujadili Kilimo hai.

 
Na Irene Mark, Dodoma

SERIKALI imeahidi kuboresha sera na sheria za kilimo ili kukitangaza na kuhamasisha kilimo hai chenye tija na usalama wa chakula.

Kauli ya Serikali ilitolewa jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo na Chakula, Japhet Hasunga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa wadau wa kilimo hai toka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na shirika la Kilimo hai Tanzania (TOAM) kwa ufadhili wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO).

Alisema kabla ya kumalizika kwa miaka mitano ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano lazima sheria hiyo itakamika na kuanza kutumika kwa maslahi ya watanzania zaidi ya asilimia 70 waliojiajiri kwenye kilimo.

Kwa mujibu wa Waziri Hasunga, kilimo hai kinapunguza  gharama za uzalishaji kulinganisha na kilimo kinachotumia kemikali huku akisisitiza Serikali itashirikiana na wadau kuhakikisha chakula kinachotokana na kilimo hai kinazalishwa cha kutosha na kinakuwa salama.

Alisema mkutano huo umefanyika wakati muafaka kwasababu wizara ipo kwenye mabadiliko makubwa ya sera na sheria za kilimo ili taifa lifamye kilimo hai.

"Watanzania kila siku wanaongezeka hivyo lazima kuwe na kilimo cha uhakika, kabla ya miaka mitano hii kumalizika lazima tuwe na sheria ya kilimo ambayo mbali ya kujadili mambo mengine itajikita katika kukiendeleza kilimo hai.

"Mabadiliko hayo yatahusisha namna sahihi ya kuwatambua wakulima mmoja mmoja, aina ya mazao anayolima na ukubwa wa shamba lake na kutunza taarifa hizo kwemye kanzidata.

"Sheria hiyo pia itaweka utaratibu wa kuwa na bima ya mazao ili mkulima awe na uhakika wa kile anachofanya," alisisitiza Waziri Hasunga.

Alitumia furs hiyo kuipongeza TOAM, FAO na wafadhili wengine kwa kuwahamasisha, kuwatambua, kuwasajili na kuwa elekezi wakulima yalipo masoko ya bidha za kilimo hai.

Alisema, mazao ya kilimo hai yanasoko kubwa duniani hivyo Tanzania unayo jukumu la kuhakikisha inakamata soko la mazao hai duniani.


Rais wa TOAM, Jordan Gama  mkutano huo unalenga kujadili kwa kina changamoto na mafanikio yaliyopo kwenye sekta ya kilimo hai na kutoa mapendelezo ya nini kifanyike ili kukinoresha.

"Dhumuni la kongamano hili litakalofanyika kwa siku mbili hapa Dodoma ni kuwaleta wadau mbalimbali wakiwamo watunga sera, wasimamia sheria,kanuni na miongozi, wanasiasa, watoa uamuzi, wazalishaji, wanunuzi na wadau wengine kutumia nafasi hiyo kwa kina kujadiliana, kupeana habari na kubadilisha maarifa kuhusu kuendeleza kilimo hai nchini," alisema.

Wadau katika mkutano huo  wataangalia kwa kina kuhusu kilimo hai kwa Tanzania , Afrika na Duniani kwa ujumla ili kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa mazao kupitia kilimo hicho ambacho kimsingi kina mafanikio mengi makubwa na wakati huo huo kunachangamoto zake.

Alisema baada ya majadiliano, wadau hao watatoka na mapendekezo ambayo yatapelekwa kwa Serikali kwa ajili ya kupata mfumo mzuri wa kuendeleza kilimo hai nchini.

Mwenyekiti wa Kamati Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mahmoud Mgimwa alisema sera ya kilimo hai ipo lakini hakijafanikiwa vya kutosha hivyo Serikali inapaswa kuisimamia ili ieleweke na kutumika ipasavyo na kushauri kiwepo na Kitengo rasmi cha kilimohai.

No comments:

Post a Comment

Pages