HATIMAYE
kibuyu kimelia huko Msimbazi, Uongozi wa klabu ya Simba umevunja
mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu klabu ya Simba kwa madai ya utovu wa
nidhamu.
Simba wamefikia hatua hiyo ikiwa ni baada ya taarifa za kufukuzwa mbelegiji huyo kushika kasi kwa muda sasa.
Aussems
ameitumikia Simba kwa misimu miwili na robo na kufanikiwa kuwapatia
Makombe mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara VPL, Ngao ya jamii na
kufanikiwa kuifikisha hatua ya Robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika CAF
CL msimu uliopita.
Kwa
Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu Auseems amefukuzwa kwa
utovu wa nidhamu kushindwa kuheshimu sehemu ya kazi na kuondoka kituo
cha kazi bila taarifa.
Kwa sasa aliyekuwa msaidizi wake Denis Kitambi atakaimu nafasi yake huku Uongozi kufanya jitihada za dhati kumpata Kocha Mkuu.
No comments:
Post a Comment