Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 30 Novemba 2019 kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dar es Salaam.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesisitiza marufuku yake aliyoitoa
hivi karibuni kuhusu ajira kwa watoto ambao wapo chini ya miaka 18.
Mhe
Hasunga amepiga marufuku hiyo leo tarehe 30 Novemba 2019 wakati
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika
ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam.
Alisema
kuwa suala la ajira kwa watoto ni miongoni mwa mambo yanazuiliwa kwenye
Sheria za kimataifa kupitia Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization) na Sheria za Ajira hapa nchini hivyo mdau yeyote atakayebainika kukiukwa maelekezo hayo atashtakiwa.
“Nawasihi
wadau wote hususani wakulima wa Tumbaku tuendelee kupiga vita ajira kwa
watoto kwa kuwa ni eneo ambalo limeendelea kulalamikiwa na wadau wengi”
Alikaririwa Mhe Hasunga
Kadhalika,
Mhe Hasunga alisema kuwa katika kuhakikisha zao la tumbaku linaendelea
kutoa mchango mkubwa katika pato la mkulima na Taifa, Wizara imejiwekea
malengo ya haraka yanayopaswa kutekelezwa ambayo ni pamoja na usajili wa
wakulima wote wa tumbaku, kuwapatia vitambulisho na kuwaingiza kwenye
kanzidata ili kupata takwimu za uhakika za maeneo wanayolima na
kuiwezesha serikali kusimamia upatikanaji wa pembejeo kulingana na
mahitaji yao.
No comments:
Post a Comment