Na John Marwa
TIMU
ya Taifa, 'Taifa Stars' leo inashuka dimbani kumenyana na Libya mchezo
kwa kundi J kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021)
Cameroon, katika mji wa Tunis nchini Tunisia kuanzia majira ya saa 4:00
usiku.
Stars wanashuka kwenye
mtanange wa leo wakiwa na mzuka wa ushindi walioupata hapa nyumabni
Novemba 15 Uwanja wa Taifa dhidi ya Equatorial Guinea kwa mabao 2-1.
Mpambano
huo wa leo unatarajiwa kuwa wenye upinzani mkubwa kutokana na Libya
kupoteza mechi yao ya kwanza dhdi ya Tunisia kwa mabao 4-1 hapo hapo
Tunisia.
Stars
wanahitaji kuibuka na ushindi ili kujiweka vema kufuzu fainali hizo kwa
mara ya pili mtawalia baada ya kufanya hivyo katika fainali zilzopita
baada ya miaka 39 walipifuzu kwa mara ya kwanza na kama watafanikiwa
kufanya hivyo itakuwa ni mara tatu Tanzania kucheza fainali hizo hapo
2021 nchini Cameroon.
Stars
wanaingia kwenye kabumbu hilo wakiikosa huduma ya mchezaji mwandamizi
Erasto Nyoni ambaye anauguza majeraha aliyoyapata dhdi ya Equatorial
Guinea.
Lakini pia Stars
chini ya Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije watakuwa wanahitaji ushindi wa
pili mfululizo tangu alipotangazwa kuwa Kocha Mkuu na watatu mtawalia
tangu ashike mikoba ya kuinoa Stars.
Wakati Stars wakiwa wageni wa Libya, Tunisia wao wamesafiri hadi Equatorial Guinea kuwavaa katika mchezo mwingine wa kundi J.
Hata
hivyo wachezaji wa Stars wamesema wanatambua umuhimu wa kupata matokeo
chanya katika mchezo huo na kuahidi kutowaangusha Watanzania usiku wa
leo.
Stars tayari
imetinga hatua ya makundi kufuzu Fainali za kombe la Dunia 2022 Qatar,
pia imefuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN
2020, CAMEROON).
No comments:
Post a Comment