Mshambuliaji
wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara ‘Kilimajaro Queens’,
Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ akiwania mpira na beki wa timu ya taifa ya
Burundi katika mchezo wa michuano ya Chalenji kwa wanawake uliofanyika
kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jana. Kilimanjaro Queens
ilishinda 4-0. (Picha na TFF).
Mshambuliaji
wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara ‘Kilimajaro Queens’,
Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ akimchambua mlinda mlango wa timu ya taifa ya
Burundi katika mchezo wa michuano ya Chalenji kwa wanawake uliofanyika
kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jana. Kilimanjaro Queens
ilishinda 4-0. (Picha na TFF).
Na John Marwa
TIMU
ya Taifa ya Wanawake Kilimanjaro Queens imezidi kuchanja mbuga katika
michuano ya CECAFA Women Senior Championship 2019 kwa kuwachakaza
Burundi kwa mabao 4-0.
Unakuwa
ushindi wa pili mfululizo kwa Kilimanjaro Queens katika hatua ya
makundi ya michuano hiyo ya Afrika Mashariki na kati kwa Wanawake
inayoendelea katika Viwanja vya Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.
Mabao
ya Kilimanjaro Queens yamewekwa kambani na Donesia Minja akiweka
kambani mabao mawili dakika za 34 na 65, Asha Rashid Mwalala dakika ya
72 na , Mwanahamis Omari 'Gaucho' dakika ya 86.
Kwa ushindi huo Kilimanjaro Queens wamefikisha pointi 6 mechi mbili na mabao 13 wakiwa hawajaruhusu bao.
Safari
ya mwisho katika hatua ya makundi kwa Kilimanjaro Queens wataumana na
ndugu zao Zanzibar Novemba 20, ambao wako dhofulihali wakiwa wameaga
mashindano hayo kwa kupoteza mechi mbili mtawalia kwa jumla ya mabao 10.
Zanzibar
walikubali kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Burundi mchezo wa ufunguzi
kisha leo kulala kwa kipigo kama hicho dhidi ya Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment