November 18, 2019

Tuzo ya The Kaizirege Excellency Award kutolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri

Waziri wa Viwanda na Biashara (kulia), Innocent Bashungwa, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shule za Kaizirege na Kemibozi, Yusto Ntagarinda Kaizirege.
 

Na Alodia Dominick, Bukoba

Mkurugenzi wa Jumuia ya Shule za Kaizirege na Kemibozi zilizopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ameanzisha tuzo kwa wahitimu wa kidato cha nne na darasa la saba watakaoingia kumi bora ya wanafunzi katika ushindi wa mitihani ya mwisho ngazi ya taifa.

Akisoma risala Meneja wa shule za Kaizirege na Kemibozi katika mahafari ya kidato cha nne na darasa la saba yaliyofanyika  jana  bw.Eulogius Katiti amesema kuwa,  mkurugenzi wa shule hizo Yusto Ntagarinda Kaizirege ameanzisha tuzo hiyo ijulikanayo kama, The Kaizirege Excellency Award ambayo itatolewa kwa wanafunzi wahitimu watakaoshinda mitihani na kuingia wanafunzi kumi bora kwa kuwasomesha bure miaka miwili.

Amesema lengo la Tuzo hiyo ni kuongeza ufauru kwa wanafunzi shuleni hapo ili waendelee kuongeza bidii katika masomo yao richa ya shule hizo kuwa na ufauru mzuri ambapo kwa mwaka jana katika matokeo ya darasa la saba  walikuwa wa tatu  Kitaifa.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafari hayo waziri wa uwekezaji na viwanda Innocent Bashungwa amewasihi wanafunzi wanaobaki shuleni  kuwa watiifu kwa wazazi/walezi na walimu wao pia washirikiane katika masomo yao na wasome kwa bidii.

Changamoto ya barabara inayokwenda katika shule hizo ambayo imetajwa katika risara ya shule, waziri Bashungwa ameahidi kuwasiliana na wahusika ili awafikishie kero hiyo na hatimaye iweze kupatiwa ufumbuzi.

Katika risala ya wahitimu wa kidato cha nne mwaka huu iliyosomwa na Walda Rushaka amesema kufauru kunahitaji kujishughulisha na kuweka jitihada katika masomo na kuwa wahitimu walianza kidato cha kwanza mwaka 2016 na kuwa wamehitimu mwaka huu wakiwa 260 wa kike wakiwa100 na wa kiume 160.

Naye msoma risara kwa wahitimu wa darasa la saba Julia Josephat amesema l wahitimu wa darasa la saba ni 80 na wanatarajia wote watashinda mtihani wao wa kuingia kidato cha kwanza.

No comments:

Post a Comment

Pages