Katika
kutambua umuhimu wa vijana ambao ni Taifa la kesho, Wanafunzi wa kidato cha
sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es
Salaam, wamepata elimu ya fedha na umuhimu wa matumizi makini ya fedha ikiwemo
kuweka akiba benki, walipotembelea Makao Makuu ya benki hiyo kujionea shughuli
mbalimbali za kibenki kwa vitendo.
Wanafunzi
wakipata elimu kutoka kwa Ofisa wa benki ya NMB- Monica Job.
Wanafunzi
hao walipata nafasi ya kujifunza na kutembelea idara na vitengo tofauti ili
kufahamu shughuli zao lakini pia walitembelea Tawi la NMB Ohio.
Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.
Pamoja
na hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amewaasa wanafunzi hao
kuwekeza nguvu zaidi katika elimu, kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza
malengo yao.
Baada
ya mafunzo hayo, wanafunzi wote walipata nafasi ya kufungua akaunti
zitakazowawezesha kutunza fedha na kujijengea tabia ya kuweka akiba na
kunufaika na huduma na bidhaa za benki ya NMB hususan Chipukizi na Mwanachuo
Akaunti.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment