Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wapili kushoto) akitoa maagizo kwa
uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania leo Jijini Dar es Salaam ya kutoa elimu kwa wadau wa tasnia ya filamu
kuzingatia maadili ya kitaaluma wapoigiza kulingana taaluma mbalimbali
ilikuzipa kazi zao mvuto, (watatu kulia) ni Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo.
Anitha Jonas – WHUSM, Dar es
Salaam
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amegiza uongozi wa Bodi ya Filamu
Tanzania kuhakikisha unatoa mafunzo kwa wadau wa tasnia ya filamu katika
kuzingatia maadili ya kitaaluma.
Dkt.Possi ametoa agizo hilo leo Jijini
Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania kwa lengo la
kufuatilia utekelezaji wa shughuli zao pamoja na uandaaji wa Marekebisho ya Kanuni za Sheria ya Bodi ya
Filamu na Michezo yakuigiza.
“Kumekuwa na changamoto kubwa kwa
baadhi ya kazi za filamu kukosa uhalisia katika maigizo ya kitaaluma haswa pale
wanapoigiza kuhusu taaluma mbalimbali mfano Madaktari,Wanasheria au Wahandisi na hii
inapelekea kupoteza mvuto wa filamu hizo,”alisema Dkt. Possi.
Akiendelea kuzungumza Dkt.Possi
alisistiza kuwa bodi inapashwa kuandaa mradi utakaosaidia wadau watasnia hiyo
kupata elimu na pia kuipaisha tasnia hiyo katika nyanja mbalimbali ikiwemo ngazi za kimataifa na kuimarisha
uandaaji wa kazi hizo kwa kuwa na viwango vyenye ubora.
Nae Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo alisema kuwa Bodi inampango wa kuanzisha programu ya kuwa na filamu ya mwezi ya kitanzania ambapo
filamu hiyo itapigiwa kura na watanzania na baada ya kushinda itazinduliwa
katika Majumba ya Sinema nchini na kwenye vingamuzi kadhaa nchi nzima na
kuonyeshwa siku moja katika muda mmoja lengo ikiwa ni kuzitafutia masoko filamu
za kitanzania na kukuza kipato cha wanatasnia wa filamu.
“Bodi inampango wa Kuanzisha Kanzi
Data ya Waandaji wa kazi za Filamu,Wasambazaji,Waigizaji,Waongozaji na
Waandishi wa Miswada ya Filamu lengo likiwa kupata takwimu zao, ili kuwa na
njia rahisi ya kuweza kuwasaidia kiuchumi wadau hawa ili angalau waweze kupata
bima ya afya au kuwasaidia kupata mikopo,”alisema Dkt.Kilonzo.
Pamoja na hayo nae Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Bibi.Joyce Fisoo aliishauri
Bodi kutumia tovuti yake katika kipindi cha kupigia kura filamu bora ya
mwezi ili kuweza kuitangaza tovuti hiyo kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment