HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 09, 2019

Butiku awataka wanataaluma kuendelea kuzungumzia suala la Katiba mpya

Na Janeth Jovin

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu nyerere, Joseph Butiku, amewataka wanataaluma nchini kuacha uoga na kuendelea kuongelea mchakato wa upatikanaji wa katiba nchini kwa Sababu ni jambo lililochukua fedha nyingi wakati wa uandaaji wake.

Pia amesema kukosekana kwa ajira nchini kumesababisha wanataaluma wengi kukimbilia katika kuwania nafasi za ubunge na uongozi Katika vyama vya upinzani kwa kuiba kura na kutoa rushwa.

Butiku ameyazungumza haya Dar es Salaam Jana katika kumbukizi ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyoandaliwa na Jumuiya ya wanataaluma  Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDASA) ikiwa na kauli mbiu ya miaka 58 ya Uhuru wajibu na mchango wa wanataaluma katika maendeleo ya Taifa.

Anasema miongoni mwa watu 30 walioanzisha mchakato huo wa katiba hadi sasa wananyooshewa vidole kutokana na kushindwa kukamilika ni yeye pamoja na Jaji Joseph Warioba .

Anaema  wasomi na wanataaluma wengi wanaomaliza wamekuwa wakikosa ajira hali inayopelekea kujidumbukiza katika kuania nafasi za ubunge jambo ambalo linatafsiriwa kuwa vyuo vinafundisha wala rushwa,wezi na mafisadi.

"Mnajua kwanini wanaandaliwa wat u wengi ambao hawawezi kuajiliwa na je  mnafahamu wanakwenda wapi watu hao Kama wanataaluma tumeweka mawazo yetu katika kutafuta ufumbuzi katika suala hilo,"alihoji Butiku na kuongeza kuwa

"Mfano nyumbani kwangu ninamwanasheria amemaliza Chuo na anamiaka minne hana kazi nimekuwa namwambia aende kijijini akajenge kibanda ili atoe ushauri wa kisheria lakini anasema anamatumaini atapata kazi mjini....hali hii inapelekea watoto wetu Kuona kazi ni kuwa wabunge na kutafuta uongozi katika nafasi za upinzani,"anasema

Butiku anasema ili kukomesha tatizo la ajira nchini ni muhimu sasa serikali  kuangalia au kubadilisha mitaala ya elimu kuanzia shule za awali hadi sekondari.

Akizungumzia kuhusu masuala ya Uchaguzi, Butiku anasema utaratibu wa upatikanaji wa viongozi nchini upo kwa mujibu katiba lakini kumekuwepo na matatizo mengi kipindi cha uchaguzi.

Anasema anashangazwa na wanataaluma kukaa kimya na kutozungumza  matatizo yanayotokea katika uchaguzi jambo ambalo halitaweza kufanikisha kuendelea na uchaguzi wa amani .

"Tunajua uchaguzi wa kupata uongozi unautaratibu wake na uchaguzi pia no eneo la maendeleo linalifanikisha upatikanaji wa viongoxi katika nchi na linasimamiwa na wanataaluma  hivi vurugu inayotokea sasa hivi inatoka wapi?,"aliuliza Butiku.

Kwa upande wake Mwanazuoni,Prof.Issa Shivji anasema ni muhimu vijana kujua historia ya nchi ili wasije Kuon a vinavyofanyika ni vigeni.

Anasema kama vijana wanataka kuleta mabadiliko wanapaswa kutosifia kila kitu bali wanapaswa kuwa watafiti na wakweli katika mambo mbalimbali.

"Kama alivyosema Butiku hauwezi kuwa jasiri kama wewe ni muoga hivyo nilazima vijana wetu wafundishwe historia ya nchi hii iliwajue tulipotoka kama nchi na tulipofika sasa,"anasema

No comments:

Post a Comment

Pages