HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2019

COSTECH NA DIT WAANZISHA MFUMO WA KUMBUKUMBU ZA BIOANUAI

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Amos Nungu (kushoto), akikabidhiana hati za ushirikiano wa pamoja wa kuwa na mfumo wa kumbukumbu za bioanuai na Makamu Mkuu wa Chuo cha Teknolojia (DIT) anayeshughulikia Utawala Dk. Najat Mohamed jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanasheria wa DIT, Nelson Ndelwa. (Picha na Goodluck Hongo).

 Na Goodluck Hongo
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk.Amos Nungu amesema uwepo wa mfumo thabiti wa kumbukumbu za  aina za viumbe na mazingira yake(Bioanuai) utasadia zaidi katika ukuzaji wa uchumi kupitia sekta ya utalii.

Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini makubaliano na Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa ajili ya kuendeleza mradi wa uhifadhi wa kumbukumbu wa Bioanuai.

Alisema COSTECH kwa kushirikiana na DIT wameandaa mkakati wa kuwa na mfumo maalumu ambao utakuwa na taarifa zote muhomu kuhusu Bioanuai zilizo nchini ili kusaidia katika upangaji wa sera na sheria za nchi kwa ajili ya ukuzaji wa uchumi

Alisema baadhi ya Bioanuai zilizopo nchini ni pamoja na Vyura wa Kihansi lakini pia eneo lenye Vipepeo huko Kusini hivyo uwepo wa taarifa rasmi za Bioanuai hizo utsaidia uongezeko la utalii na kuinua uchumi wan chi yetu.

“Leo tumekutana hapa na wadau wote wa Bioanuai wakiwemo wakuu wa taasisi mbalimbali zinazojihusisha na suala hali hii na lengo kuu ni kuwa na mfumo wa maalumu wa kuweka kumbukumbu  na kuainisha mahali zilipo”amesema Dk. Nungu.

Dk.Nungu aliongeza kuwa COSTECH ndio inayoratibu mfumo huo lakini DIT ndio waliotengeza hivyo wao wanaishukuru Serikali na wadau wengine katika kukuhakikisha watanzania wanapata maendeleo.

“Tunakuwa na utajiri mwingi wan chi lakini sisi hatujui hivyo hiyo ni hasara kwa Taifa lakini taarifa zikiwa wazi basi tunaweza kuongeza utalii zaidi kupitia Baianoai zilizopo nchini”amesema Dk.Nungu
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha DIT,Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Utawala Dk.Najat   Mohamed alisema bila Bioanuai hakuna maisha  hivyo uwepo wa viumbe hai na mazingira yake utasadia kuimarisha mipango ya Serikali katika ukuzaji wa uchumi

“Bioanuai ndio chanzo cha chakula,madawa na ma mambo mengine mengi hivyo basi kutokana na umuhimu wake DIT iliamua kutengeneneza mfumo huo ili kuwepo na kumbukumbu zake”amesema Dk.Mohamed

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Ikolojia na Uhifadhi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof.Pantaleo Munishi amesema Bioanuai ni msingi wa maisha ya binadamu hivyo uwepo wa taarifa rasmi za kumbukumbu zake utasaidia katika mipango ya maendeleo.

“Bioanuai kwa ufupi ni aina zote za viumbe walio nchi kavu na baharini pamoja na mazingira yao wanayoishi,hivyo hapo kuna mazao ya Kilimo,Misitu yakiwemo na majini hivyo tukiacha hali hiyo ipotee basi tutaharibu uchumi wetu”amesema Prof. Munishi

No comments:

Post a Comment

Pages