Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Amos Nungu
(kushoto), akikabidhiana hati za ushirikiano wa pamoja wa kuwa na mfumo wa
kumbukumbu za bioanuai na Makamu Mkuu wa Chuo cha Teknolojia (DIT)
anayeshughulikia Utawala Dk. Najat Mohamed jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mwanasheria wa DIT, Nelson Ndelwa. (Picha na Goodluck Hongo).
Na Goodluck Hongo
Na Goodluck Hongo
MKURUGENZI
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk.Amos Nungu amesema
uwepo wa mfumo thabiti wa kumbukumbu za
aina za viumbe na mazingira yake(Bioanuai) utasadia zaidi katika
ukuzaji wa uchumi kupitia sekta ya utalii.
Hayo
aliyasema jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini makubaliano na Chuo cha
Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa ajili ya kuendeleza mradi wa uhifadhi wa
kumbukumbu wa Bioanuai.
Alisema
COSTECH kwa kushirikiana na DIT wameandaa mkakati wa kuwa na mfumo maalumu
ambao utakuwa na taarifa zote muhomu kuhusu Bioanuai zilizo nchini ili kusaidia
katika upangaji wa sera na sheria za nchi kwa ajili ya ukuzaji wa uchumi
Alisema
baadhi ya Bioanuai zilizopo nchini ni pamoja na Vyura wa Kihansi lakini pia eneo
lenye Vipepeo huko Kusini hivyo uwepo wa taarifa rasmi za Bioanuai hizo
utsaidia uongezeko la utalii na kuinua uchumi wan chi yetu.
“Leo
tumekutana hapa na wadau wote wa Bioanuai wakiwemo wakuu wa taasisi mbalimbali
zinazojihusisha na suala hali hii na lengo kuu ni kuwa na mfumo wa maalumu wa
kuweka kumbukumbu na kuainisha mahali
zilipo”amesema Dk. Nungu.
Dk.Nungu
aliongeza kuwa COSTECH ndio inayoratibu mfumo huo lakini DIT ndio waliotengeza
hivyo wao wanaishukuru Serikali na wadau wengine katika kukuhakikisha
watanzania wanapata maendeleo.
“Tunakuwa na
utajiri mwingi wan chi lakini sisi hatujui hivyo hiyo ni hasara kwa Taifa
lakini taarifa zikiwa wazi basi tunaweza kuongeza utalii zaidi kupitia Baianoai
zilizopo nchini”amesema Dk.Nungu
Akizungumza kwa
niaba ya Mkuu wa Chuo cha DIT,Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia
Utawala Dk.Najat Mohamed alisema bila
Bioanuai hakuna maisha hivyo uwepo wa
viumbe hai na mazingira yake utasadia kuimarisha mipango ya Serikali katika
ukuzaji wa uchumi
“Bioanuai
ndio chanzo cha chakula,madawa na ma mambo mengine mengi hivyo basi kutokana na
umuhimu wake DIT iliamua kutengeneneza mfumo huo ili kuwepo na kumbukumbu
zake”amesema Dk.Mohamed
Kwa upande
wake Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Ikolojia na Uhifadhi kutoka Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof.Pantaleo Munishi amesema Bioanuai ni msingi wa
maisha ya binadamu hivyo uwepo wa taarifa rasmi za kumbukumbu zake utasaidia
katika mipango ya maendeleo.
“Bioanuai
kwa ufupi ni aina zote za viumbe walio nchi kavu na baharini pamoja na
mazingira yao wanayoishi,hivyo hapo kuna mazao ya Kilimo,Misitu yakiwemo na
majini hivyo tukiacha hali hiyo ipotee basi tutaharibu uchumi wetu”amesema
Prof. Munishi
No comments:
Post a Comment