Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia kwa waliosimama kwa nyuma), Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut Binsar Panjaitan (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa kwanza kulia) wakishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano Jijini Dodoma baina ya Kampuni ya PT Wijaya Karya (WIKA)ya Indonesia na Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA-Afrika) mapema leo tarehe 17 Desemba, 2019 Jijini Dar es Salaam. Wanaosaini makubaliano hayo ni Mtendaji Mkuu wa WIKA Bw. Destiawan Simeon (kushoto) na Katibu Msaidizi wa CPA Afrika Bw. Said Yakubu.
Mtendaji Mkuu wa WIKA Bw. Destiawan Simeon (kushoto) na Katibu Msaidizi wa CPA Afrika Bw. Said Yakubu, akibadilishana hati ya makubaliano ya awali ya ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa WIKA Bw. Destiawan Simeon (kushoto) na Katibu Msaidizi wa CPA Afrika Bw. Said Yakubu, akibadilishana hati ya makubaliano ya awali ya ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Kampuni ya WIKA, Bw. Destiawan Simeon (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Absolomon Shausi wakisaini mkataba wa kuingia ubia wa kujenga Miradi Mikubwa ya Miundombinu ndani ya SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo itajumuisha Miradi ya umeme, barabara, reli, madaraja, viwanja vya ndege na majengo mbalimbali.
Mwakilishi wa Kampuni ya WIKA, Bw. Destiawan Simeon (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Absolomon Shausi , wakibadilishana hati ya mkataba wa ubia wa kujenga Miradi Mikubwa ya Miundombinu ndani ya SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo itajumuisha Miradi ya umeme, barabara, reli, madaraja, viwanja vya ndege na majengo mbalimbali.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya TIMMAH, Bw. Trenggono Sutioso, akisaini Mkataba wa Ushirikiano kwenye Kuchimba na Kuchakata Madini na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki (wa tatu kulia waliosimama), Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (kulia).
No comments:
Post a Comment