Nahodha Msaidizi wa Timu ya Bunge la Tanzania "Bunge Sport
Club," Omary Mgumba, akijiimarisha kimazoezi kabla ya timu yake kukutana
na wenyeji wa Uganda, kwenye Uwanja wa KCC jijini Kampala.
Na Mwandishi Wetu, Kampala
MICHEZO ya Mabunge ya Afrika Mashari yamehitimishwa, huku timu ya Bunge la Tanzania ikishinda nafasi ya pili.
Michuano hiyo iliyoanza Desemba 8,2019, kisha kumalizika 18 Desemba, jijini Kampala, Uganda.
Katika michuano hiyo, timu mwenyeji ya Bunge la Uganda,
ndiyo iliyonyakua ubingwa wa mashindano hayo ya Mabunge ya Afrika
Mashariki.
Nahodha Msaidizi wa timu ya mpira wa miguu ya Bunge la
Tanzania, 'Bunge Sport Club,' Omary Mgumba, aliwapongeza wabunge wenzake
kwa ushindi.
"Ushindi wa nafasi ya pili ni mkubwa. Tunajivunia ingawa nafsi zetu tulitaka tuongoze, lakini hakuna noma.
"Tutajiandaa michuano ijayo mwaka 2020 pale Arusha nyumbani kwetu," Nahodha Msaidizi Mgumba, alisema.
Timu ya Bunge la Tanzania ilirejea nchini juzi, ikitokea Kampala ilikokipiga na kuweka historia katika medali ya michezo.
Kwa mujibu wa Nahodha huyo Msaidizi, mashindano hayo ni matakwa na masharti ya Jumuita ya Afrika Mashariki.
Lengo lake ni kujenga umoja, mshikamona na upendo miongoni mwa wabunge na raia wa jumuiya hiyo.
Afrika Mashariki inaundwa na mataifa ya Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Sudan Kusini.
"Mashindano haya mwakani yatafanyika nchini kwetu. Tanzania ni wenyeji pia wa Bunge la Jumuiya ya Africa Mashariki (EALA).
"Tutaimarisha mazoezi chini ya kocha wetu mheshimiwa
Mwamoto, kwa uangalizi na malezi ya Spika wetu, Job Ndugai, chini ya
Serikali," alisema.
"Mashindano haya mwakani yatafanyika nyumbani, jijini
Arusha," alisisitiza Mgumba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo na
Chakula.
Alisema kuwa, pamoja na mambo mengine michuano hiyo itaanza
kutimua vumbi Desemba,2020, muda mfupi baada ya Uchaguzi Mkuu
kumalizika.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Bunge la Uganda, waliwasifu
wabunge wa Tanzania kwa namna walivyotoa ushindani mkali kwenye michuano
hiyo.
"Ni wazuri kila idara, ila sisi ndiyo kiboko yao," alisikika akisema mmoja wa wabunge wa Uganda.
No comments:
Post a Comment