HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 20, 2019

INDONESIA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA MADINI MKOANI KAGERA


 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, akimsikiliza Balozi wa Indonesia Prof. Ratlan Pardede.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, akibadilishana mawazo na Balozi wa Indonesia Prof. Ratlan Pardede.
 

Na Lydia Kugakila, Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, amewataka wananchi mkoani Kagera kutumia vizuri fulsa ya kujiunganisha kibiashara na nchi ambazo zishapiga hatua kubwa katika sekta ya biashara

Brigedia Jenerali Gaguti ametoa kauli hiyo wakati akimpokea Balozi wa Indonesia Prof. Ratlan Pardede, ambaye yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuona fulsa mbali mbali zinazoweza kuunganisha mkoa wa Kagera na nchi ya Indonesia kibiashara hasa  katika sekta ya madini hapa nchini.

Akitaja malengo ya Balozi huyo kufika hapa nchini Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema ujio wa Balozi Pardede katika suala la uwekezaji  katika sekta ya madini ya tini kutasaidia kupata wawekezaji zaidi kwani kipindi cha nyuma kumekuwepo na changamoto ya watu kujichimbia madini bila kufuata utaratibu jambo ambalo limekuwa likisababisha madini kutoroshwa.

Amesema malengo  hayo ya Balozi wa Indonesia yatasaidia kupata kuongeza thamani hapa nchini na kupunguza adha kwa wananchi wanaotorosha madini kwa njia ya panya na kutoa nafasi kwa nchi jirani kuleta madini yao kufanyiwa uongezaji wa thamani katika nchi ya Tanzania ili kuongeza pato la Taifa kupitia madini.

Balozi huyo amepata nafasi ya kukutana na jumuhiya ya wafanyabiashara wa mkoa huo na kubadilishana mawazo na kuona ni namna gani ya watapanga pamoja biashara na kujikita katika kutembelea maeneo ya mkoa huo hasa wilaya ya Kyerwa yanakopatikana madini ya tini.

Balozi Pardede amesema nchi ya Indonesia ina uzoefu katika masuala ya madini kwa hiyo ushirikiano kati ya nchi ya Indonesia na Tanzania ni wa kudumishwa ili kuongeza uchumi wa pato la madini kwa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake afisa madini mkoa wa Kagera mhandisi Lucas Mlekwa amesema mkoa wa Kagera una kiwanda cha madini kimoja na kuwa ujio wa wawekezaji utaweka nguvu kubwa huku utafiti ukizidi kufanyika ili kujua kiwango cha tini kilichopo wilayani Kyerwa ili kukuza uchumi wa mkoa.

Ametaja changamoto zilizopo katika sekta hiyo kuwa ni pamoja na sheria inayotaka madini yote kuongezewa thamani na kuwa tayari kiwanda cha kuongeza thamani kimepatikana kimoja na kuutaja mkoa wa Kagera kuwa na madini mengi.

Ameongeza kuwa katika takwimu zipo leseni 655 za wachimbaji wadogo kwa madini yote yanayopatikana Mkoani Kagera na kwa madini ya tini zipo leseni 257 za wachimbaji wadogo huku leseni za utafiti zikiwa 26.

No comments:

Post a Comment

Pages