Na Janeth Jovin
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Temeke, imemkamata karani wa Mahakama ya mwanzo ya mkoa huo Levina Mboya kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 200,000.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Mkuu wa Takukuru mkoa huo, Ramadhani Ndwatah (pichani), anasema uchunguzi walioufanya ulibaini Novemba 11 mwaka huu saa 11 jioni, Mboya akiwa ofisini kwake alipokea fedha hizo za mtego ili aweze kumsaidia mwananchi mmoja kupata nakala ya mwenendo wa kesi ili akate rufaa.
Anasema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo umekamilika na mtuhumiwa huyo amefikishwa leo mahakamani na kufunguliwa mashitaka kwa kosa la kushawishi, kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na 11 ya mwaka 2007.
"Tunaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia mitandao yote ya simu kwa kupipa au kutuma ujumbe mfupi kwa namba ya bure 113 au kupiga 113 au kufika ofisi za Takukuru iliyopo karibu nawe," anasema.
Aidha anasema bado Temeke imekuwa ikilalamikiwa kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika masuala ya ardhi hivyo bado wanaendelea na uchunguzi na watatoa taarifa hivi karibu juu ya watu wanaohusika na vitendo hivyo.

No comments:
Post a Comment