December 14, 2019

Kifaa cha kudhibiti wizi wa bodaboda na vyombo vya moto chazinduliwa

Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni  inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali ya kiteknolojia ya MD Technology,  Mohamed  Kaddy akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Baadhi ya madereva bodaboda wakipokea maelezo kutoka kwa Kampuni ya uundaji wa mifumo mbalimbali ya kiteknojia ya MD Technology ambayo imezindua kifaa cha kudhibiti wizi wa pikipiki.
 

Na Janeth Jovin

KAMPUNI inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali ya kiteknolojia ya MD Technology imezindua kifaa maalumu chenye uwezo wa kuthibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho, Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, Mohamed  Kaddy, amesema kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana kwa kuwa itaonekana eneo iliyopo.

“Ni teknolojia rahisi itakayodhibiti wizi wa pikipiki ambao sasa ni moja ya matatizo sugu yanayolalamikiwa na wateja wengi.Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi, itapatikana tu, lakini pia kama kuna mtu amesimama katika pikipiki yako utajulishwa”alisisitiza Kaddy katika uzinduzi huo.

Anasema kifaa hicho maalum kitafungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja atapata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika siku yake ya mkononi.

Alifafanua kuwa mfumo huo usaidia kudhibiti udanganyifu wa madereva au marafiki katika matumizi ya umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.

“Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki kupata taarifa kwa haraka pale chombo chake kikitaka kuibiwa au kushikwa na mtu, pia mfumo huo utamsaidia mtu kuzima au kuwasha chombo mahali popote atakapokuwa, kama umeibiwa unauwezo wa kuizima pikipiki yako kabla haijafika mbali," anasema

Anasema kifaa hicho tayari kimeshaanza kuuzwa na kinapatika kwa bei ya Sh. 150,000 hivyo madereva wajitokeze kwa wingi kununua ili kudhibiti wezi.

1 comment:

Pages