December 14, 2019

WAZIRI UMMY AZINDUA BODI YA WADHAMINI-MOI

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Sheria na Mpango mkakati wa MOI Mwenyekiti mpya  wa Bodi ya wadhamini Prof. Charles Mkony.


Na Asha Mwakyonde

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa tangu serikali ya awamu ya tano ilivyoingia madarakani malalamiko mengi yamepungua na kwamba yaliyobaki ni kwa upande wa gharama za matibabu.

Pia ameitaka bodi mpya chini Mwenyekiti wake wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Prof. Charles Mkony,  kusimamia changamoto zikiwamo za upungufu wa madaktari bingwa.

Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam leo Disemba 13, 2019 wakati akizindua bodi mpya ya Taasisi hiyo amesema anaimani na bodi hiyo itasimamia vizuri utekelezaji wa kila siku.

 Amesema kuwa taasisi ya MOI ina madaktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu saba na kwamba wanaohitajika ni 13 na wausingizi waliopo ni watano huku wanaohitajika ni 15 na nchi nzima hawafiki 30.

Naye Mkurugenzi wa Mtendaji wa taasisi hiyo Dk. Respicious Boniface amsema imewafanyia upasuaji mbali mbali wa kibingwa wagonjwa 43,200 katika kipindi cha awamu ta tano.

Akifafanua  kuwa upasuaji huo umefanyika kwa wagonjwa wa Kubadilisha nyonga 900 Kubadilisha magoti 870, upasuaji wa mfupa wa kiuno 618 upasuaji wa Ubongo 880 na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi 2,070.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa gharama za matibabu hayo ndani ya nchi zilikua Shilingi za Kitanzania bilioni 16.5.

"Wagonjwa haww kama  wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya shilingi bilioni 54.9 zingetumika," amesema Dk.Boniface.

Ameongeza  kuwa tasisi hiyo imeokoa shilingi bilioni 38.4, ambazo zitatumika kwa shughuli nyingine za maendeleo ya
nchi.

Kwa upande mwenyekiti huyo Prof. Mkony amesems kuwa tayari bodi hiyo imeshanza kutatua baadhi ya changamoto ikiwamo ya kupata eneo la kujenga kituo cha MOI kitakachokuwa  Mbweni  Wilayani Kinondoni.

"Kituo hiki kitasaidia kipunguza msongamano wa wagonjwa na badala yake watatibiwa huko huko na jana tumepokea hati miliki ya eneo hili hivyo kituo hicho kitaendelea kujengwa,",amesrma Prof.  Mkony.

Prof. Mkony ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kufanya uteuzi wa bodi hiyo mchanganyiko wanaume na wanawake.

No comments:

Post a Comment

Pages