Msafara wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' umetua salama nchini Uganda tayari kwa mashindano ya CECAFA Challenge 2019.
Stars ambayo imepangwa kundi B la mashindano hayo sambamba na timu za Kenya, Sudan na Zanzibar iliwasili nchini hapa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Entebe, kwa ndege ya Shirika la Uganda 'Uganda Airlines' mnamo saa 11.15 jioni.
Mara baada ya kuwasili, msafara huo ulipokelewa na Ofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Richard Ssemanda na kuelekea moja kwa moja katika hoteli ya G One iliyopo jijini Kampala.
Hoteli hiyo pia ndio imefikia timu ya taifa yaZanzibar 'Zanzibar Heroes'
Msafara wa Stars unahusisha wachezaji 22, maofisa tisa wa benchi la ufundi na viongozi watano.
Muda mfupi baada ya Stars kutua, nyota anayechezea Difaa el Jadida ya Morocco, Nickson Kibabage aliungana na wenzake kikosini.
Imetolewa na Idara ya Habari ya TFF

No comments:
Post a Comment