Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, akitoa neno kwa wenyeviti wa
serikali za mtaa na wajumbe.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, amesema kuwa ameanzisha kampeni ya
utoaji tuzo kwa mitaa itakayofanya vizuri kwenye suala la usafi ambapo kila
mtaa utapatiwa zawadi ya fedha tathilimi.
Aidha Mhe.
Chongolo amewaonya wananchi wanaotupa taka hovyo na hivyo kuwataka watendaji
hao kusimamia sheria kwa watakaojihusisha na uharibifu huo wa mazingira ikiwemo
kulipa faini kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo, wakati wa
ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti wa serikali, wajumbe wa mitaa pamoja
na watendaji kata iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomi Ostarbey.
Mhe.
Chongolo amesema kuwa lengo la kampeni hiyo, ni kuongeza motisha katika kuboresha
Halmashauri hiyo kuwa katika muonekano mzuri, na kuwasisitiza watendaji hao
pamoja na wenyeviti wa mitaa kusimamia kwa ukamilifu.
Amefafanua kuwa
tuzo hiyo itatolewa kila maada ya miezi
mitatu ambapo mtaa utakaoibuka na ushindi itapatiwa fedha tathilimu kiasi cha
shilingi 500, 0000, mshindi wa pili 300,000 huku mshindi wa tatu akipata
shilingi 200,000.
“
Halmashauri ya Kinondoni ni safi, lakini tunatakiwa kufanya vizuri zaidi , kwa
mantiki hiyo tunakuja na kapmeni ya usafi wa kila mtaa, watakaofanya vizuri
watapatiwa zawadi ya fedha, na fedha hizo zitabaki kwenye mitaa yenu kwa ajili
ya shuguli nyingine” amesema Mhe. Chongolo.
”Watakaoendesha
mchakato huo ni nyie wenyeviti na wajumbe wa mitaa, kazi yangu mimi ni kuweka
fedha kwa ajili ya kutoa zawadi, na kampeni hiyo tunaianza leo hii arehe nne
mwezi wa 12 kwa hiyo ikifika tarehe nne mwezi watatu 2020 tutatoa tuzo hiyo kwa
mitaa itakayokuwa imeshinda.
Aidha Mhe.
Chongolo ameongeza kuwa pamoja na tuzo hizo kutolewa amewataka watendaji kusimamia sheria na kanuni za utunzaji
mazingira ikiwemo kutoza faini kwa watu wanaotupa taka hovyo kwani kwakufanya
hivyo wataongeza ufanisi na ubora wa mitaa kuendelea kuwa misafi.
“ Zipo
sheria za usafi ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria lakini hazifuatwi,
watendaji, wenyeviti na wajumbe mliopo hapa nendeni mkazisimamie vizuri”amesisitiza.
Katika hatua
nyingine Mhe. Chongolo amewataka viongozi hao kusimamia mapato vizuri sambamba
na kuepuka rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutawaingiza kwenye matatizo makubwa.
“ Kunasuala
la rushwa, ni waonye msijihusishe na mambo hayo, leo hii hapa kuna maafisa kutoka
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wapo hapa nawao wata waeleza
madhara ya kupokea au kutoa rushwa, niwaombe sana msikilize kwa makini na mkayafanyie
kazi” ameongeza Mhe. Chongolo.
Kwa upande wake
Afisa utumishi mkuu wa Halmashauri hiyo Bi Faudhia Nombo amesema kuwa lengo la
mafunzo hayo elekezi ni kuwawezesha viongozi hao ili waweze kutekeleza majukumu
ya usimamizi na undeshaji wa shughuli mbalimbali katika mitaa yao kwa
kuzingatia Sera, Sheria , Taratibu ,Kanuni na miongozo iliyopo ilikuboresha
utoaji wa huduma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment