Mwanamke Mjasiliamali akifafanua jambo kuhusu bidhaa ya wine inayotengenezwa
kiwandani kwake kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati
wa ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini
Arusha kushoto kwake ni Mboni Mgaza Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya familia
kutoka Wizara ya Afya.
Na
Mwandishi Wetu, Arusha
Serikali inatambua
kuwa haiwezi kufikia malengo ya
maeandeleo endelevu ikiwa
wanawake hawatashiriki na kunufaika na uchumi kama ilivyo kwa wanaume kwasababu
mfumo dume hautoshi kuiletea Nchi maendeleo.
Hayo yamesemwa leo na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati wa ufunguzi wa Kongamano
la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha.
Bw. Kwitega ameongeza
kuwa ili kuwa na maendeleo endelevu ni lazima kuwashirikisha wanawake kiuchumi
ili kunuafaika na uchumi au matokeo ya shughuli za Maendeleo.
Aidha Bw. Kwitega
aliongeza kuwa kwa kuzingatia dhamana ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya
Jamii ya uratibu na wa masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake
kiuchumi inaendelea na maandalizi ya sera ya Jinsia ili kuhakikisha mipango
yote inazaingatia usawa wa kijinsia.
Bw. Kwitega ameitaja
mikakati na mipango ya maendeleo ya Taifa pamoja na mpango wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kuwa mipango yote iliyopo
inaielekeza Serikali kuwezesha wanawake kiuchumi.
Kiongozi huyo wa Mkoa
wa Arusha amezija juhudi za serikali katika kuhakikisha wanawake wanakua
kiuchumi kuwa ni kuhamasisha wanawake kujiunga VICOBA na SACCOS na vikundi
vingine vya hisa na kuongeza kuwa mpaka sasa serikali ina vikundi 918 venye
jumla ya Wanawake 10,708 wamejiunga na vikundi hivyo Nchi nzima.
Naye Mkurugenzi
Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mboni Mgaza amesema
lengo kuu la Kongomano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni kuwatayarisha wanawake Mkoani Arusha pamoja na Taasisis
zinazojishughulisha na uwezeshaji
wanawake kuweza kuwajenga uwezo wa
kiuchumi.
Bi. Mgaza amezitaja
mbinu zinazotumika kujengea uwezo wa wanawake kiuchumi ni pamoja na kuwapa
mitaji na mikopo lakini pia kuwapa ujuzi wa teknolojia na kujenga ubia baina ya
Serikali na Taasisi mbalimbali.
Bi. Mboni aliongeza
kuwa Kongamano hilo la wanawake linalenga vikundi vya kiuchumi, vikundi vya
ujasiliamali pamoja na watu binafsi zikiwemo taasisi mbalimbali Mkoani Arusha
kwa lengo la kupata maarifa mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi.
Serikali imekuwa
ikitoa Mikopo kupitia Serikali za Mitaa kwa Wanawake waliokatika vikundi vya
hisa na ujasiliamali kwa lengo kuwezesha wanawake kiuchumi na tayari Serikali
tayari kupitia mapato ya Halmashauri zote Ncini inatenga asilimia kumi ya
mapato yake kwa lengo la kuwezesha wanawake vijana na walemavu.
No comments:
Post a Comment