Na Mwandishi Wetu
Wataalamu
wa maabara nchini kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya
wanyamapori, mifugo na mazingira wameipongeza serikali ya awam ya tano
kwa jitihada zake za kuboresha maabara za sekta hizo kwa kuziwezesha
kuwa na vitenganishi, vifaa vya kisasa, teknolojia na kuwajengea ujuzi
wataalam hao ili kuweza kufanya utambuzi na uchunguzi ndani ya maabara.
Akiongea
wakati wa mkutano wa mwaka wa Mtandao wa wataalam wa maabara nchini
(LABSNET),Jijini Arusha, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Vetenari
Tanzania, Dkt. Furaha Mramba amefafanua kuwa kutokana na jitihada za
serikali katika kuimarisha kuboresha utendaji wa maabara nchini, tayari
maabara za hapa nchini zinao uwezo wa kutambua magonjwa yote
yanayowapata mifugo lakini pia na magonjwa yanayowapata binadamu.
“Zamani
tulikuwa tunapeleka sampuli nje ya nchi hususani katika nchi ya Kenya
na katika nchi ya Afrika kusini, lakini miaka ya hivi karibuni kutokana
na kazi nzuri iliyofanywa na serikali katika kuboresha utendaji wa
maabara tulizonazo, tayari tunazo maabara za rufaa ambazo zinauwezo
mkubwa wa kufanya utambuzi na uchunguzi wa magonjwa” Amesisitiza Dkt.
Mramba.
Dkt.
Mramba ameongeza kuwa lengo la kukutana kwa wataalam wa maabara nchini
kutoka katika sekta zote za Afya ni kujadiliana na kuona mbinu bora za
kufanya uchunguzi na kutambua kwa wepesi na kwa haraka magonjwa kabla
hayajaleta madhara makubwa kwa mifugo na binadamu. Amefafanua kuwa
katika mkutano huo wameshiriki wadau wa maendeleo katika sekta ya
maabara kutoko Marekani na Finland.
“Tunapokutana
na wadau hawa ambao hutufundisha teknolojia za kisasa za maabara na
hutupatia vifaa vyenye uwezo mkubwa wa utambuzi wanaweza kujua ni
teknnolojia gani tunaihitaji kwa sasa na maabara gani zinahitaji
kujengewa uwezo katika uchunguzi na utambuzi. Wadau hawa kwa jinsi
wanavyo unga juhudi za serikali ndio maana sekta ya maabara hapa nchini
imekuwa bora” Amesema Dkt. Mramba.
Kwa
upande wake Mratibu kutoka Finland wa Mradi unaotekelezwa hapa nchini
wa Kuimarisha Afya na Usalama katika Maabara kwa kujenga uwezo wa
Utambuzi, Dkt.Lina Voutilainen, amebainisha kuwa wamekuwa wakiunga
mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuboresha utendaji wa
maabara nchini kupitia Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania kwa
kuwajengea uwezo wataalam wa maabara na kuwapatia vifaa vyenye uwezo
mkubwa wa utambuzi na uchunguzi wa magonjwa.
“Tayari kupitia Wakala
wa Maabara ya Vetenari Tanzania tumetoa vifaa sita vya QPCR
vinavyohamishika kwa maabara zake za kanda ya Mwanza, Arusha na Iringa,
Tutaendelea kutoa vifaa hivyo vya kisasa na vitenganishi pamoja na
kuendelea kuwajengea uwezo wataalam wa maabara katika kipindi
tutakachotekeleza mradi huu hadi 2023 ” Amesisitiza Voutilainen
Naye,
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uchunguzi, kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Alex Magesa,
amefafanua kuwa katika kuhimarisha Huduma za uchunguzi imebainika kuwa
usugu wa vimelea dhidi ya dawa ni changamoto kubwa hivyo tayari serikali
imeandaa mpango mkakati wa kukabiliana na changamoto hiyo ambapo
wafamasia na wanafuzi na jamii kwa ujumla wanahusishwa katika kukabili
changamoto hiyo.
Mkutano
huo ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kupitia Dawati la Uratibu wa
Afya moja, uliwakutanisha wataalam wa maabara hao kwa kuzingatia dhana
ya Afya moja ambayo ni wataalam wa maabara kutoka sekta ya Afya ya
binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira.
No comments:
Post a Comment